……………………………………………………………………………………………….
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZA
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Yah: Salaam za Rambirambi
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za
msiba wa msanii nguli wa tasnia ya muziki wa Dansi nchini Muhidini
Maalimu Ngurumo
“
Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo
hiki cha Muhidini Maalimu Ngurumo ambaye mchango wake katika muziki wa
dansi ni mkubwa mno na unahitajika sana, pengo aliloliacha ni kubwa
kwani ubunifu wake bado unahitajika katika tasnia hii.” Baraza linatoa
pole kwa familia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha tunawatakia
moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa
wetu.
Mwenyezi
Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Baraza liko
pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Imetolewa na
Godfrey Mngereza
Kaimu Katibu Mtendaji
Baraza la Sanaa la taifa.