Mshauri wa
Biashara wa Kimataifa wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits, James
Rugemarila (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe: Fabian Masawe
alipowasili katika ofisi za Kampuni ya Mabibo Aprili 10, 2014 jijini Dar es
Salaam,kwaajili ya kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya
Uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazozinduliwa kitaifa katika Mkoa huo
ambapo uzinduzi huo utaenda sambamba na uzinduzi wa miradi mbalimbali katika
mkoa huo.wadhamini wa mbio hizo ni
Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits.
HABARI
PICHA-NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWEBLOG DAR ES SALAAM
0787 94 2222
Mwenyekiti
Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Sprits,Benedicta Rugemalira
(kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe: Fabian Masawe,
alipowasili kuzungumza na waandishi wa habari.
Kulia
ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe: Fabian Masawe (katikati), Mshauri wa Biashara wa
Kimataifa wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits, James Rugemarila, na
kushoto, Mkuu wa
Wilaya ya Muleba, mkoani
Kagera, Lembris Kipuyo wakiingia kwenye ukumbi ulioandaliwa kwaajili ya
kuzungumza na waandishi wa habari.
Mshauri
wa Biashara wa Kimataifa wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits, James
Rugemarila,akielezea machache kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa
Kagera Mhe: Fabian Masawe, kuhusiana na kuadhamini kwa mbio za Mwenge wa Uhuru.
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Mhe: Fabian Masawe (katikati), akizungumza na waandishi wa habari
kuhusina na maandalizi ya Uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazozinduliwa
kitaifa katika Mkoa huo ambapo uzinduzi huo utaenda sambamba na uzinduzi wa
miradi mbalimbali katika mkoa huo.wadhamini wa
mbio hizo ni Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits.
Mkuu
wa Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera, Lembris Kipuyo akisisitiza
kuhusina maandalizi yam bio hizo, kulia kwake ni, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe: Fabian Masawe,
Mwenyekiti
Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Sprits,Benedicta Rugemalira,
akielezea kuhusiana na jinsi walivyo
jiandaa kuhusina na mbio za Mwenge wa Uhuru.
Mshauri wa
Biashara wa Kimataifa wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits, James
Rugemarila, akisisitiza jambo.
Meneja
Mauzo wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits, Bw Kevin Costa akitambulisha
wageni mbalimbali wakati wa mkutano huo.
Waandishi wa
habari wakiwa kwenye mkutano huo.
Meneja
Masoko na Biashara wa Benki ya Mkombzi, Grace Mboya akielezea kuhusina huduma
za kibenki wakati, kushoto kwake ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo
Beer Wines and Sprits,Benedicta Rugemalira
Kulia
ni Bw: Boniface, na Rutabingwa, wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Wilaya ya Muleba, mkoani
Kagera, Lembris Kipuyo wakati akiezea kuhusiana na maandalizi ya Uzinduzi wa
mbio za Mwenge wa Uhuru.
Joe
Mgaya (kushoto), akiwa na Respicus Didace, wakifurahia jambo wakati wa Mkutano huo.
wafakazi
wa Kampuni
ya Mabibo Beer Wines and Spririt, wakiwa kwenye Mkutano huo.
........................................................................................
Dar es Salaam.Mkoa wa Kagera unategemea kutumia Bilioni 14
kwa ajili ya kuzindua miradi mbalimbali wakati wa kukimbiza mbio za Mwenge wa
Uhuru utakaozinduliwa Kitaifa Mei 2
mwaka huu.
Hayo yalibainishwa na Mkoa huo, Fabian Masawe wakati
akizungumza na waandishi wa Habari jana kuhusu maandalizi ya uzinduzi huo.
Alisema mwenge huo utakimbizwa katika halmashauri nane za mkoa
huo ambapo wananchi zaidi ya 30,000
watashiriki wakiwemo kutoka nchi za jirani na mkoa huo.
Masawe alitoa wito kwa wananchi na taasisi mbalimbali
kujitokeza kuchangia mbio hizo ili kukufanikisha uzinduzi huo.
Alisema baada ya kukimbiza katika Halmashauri hizo kuwa
mwenge huo Mei 10 mwaka huu utakabidhiwa
katika wilayani Kakongo mkoani Kigoma.
“Kauli mbiu ya mwaka huu yam bio za mwenge Katiba ni Sheria
kuu ya nchi jitokeze kupiga kura ya maoni kupata katiba mpya”,alisema Masawe.
Mdhamini wa mbio hizo,Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya
Mabibo Beer Wines and Spririt,Benedicta Rugemalira alisema watashirikin na
Serikali kudhamini sehemu y uzinduzi huo
kupitia vinywaji vyao.
Rugemalira alisema watahakikisha wanatoa huduma za vinywaji
kambacho hakina kilevi na bia ya Windhoek.
“Vinywaji hivi ni vizuri sana hivyo wananchi watafurahia sana
wakati wa uzinduzi wa mbio za mwenge utakaofanyika mkoani Kagera"










