Baada ya kusota takribani,miaka 5 mitano jela hatimaye wale
wachina waliokamatwa wakivua samaki ndani ya ukanda wa uchumi wa Tanzania wa
bahari ya Hindi
Hii ilitokea wakati Mhe John Magufuli akiwa Waziri wa Ardhi
na uvuvi.Pia mahakama imeamuru Wachina warudishiwe mali zao zote walizokamatwa
nazo ikiwemo samaki ,ambao tayali Magufuli aliamuru wagawiwe bule kwa wananchi
na Taasisi mbalimbali vikiwemo vyuo shule za kulala,Magereza nk.
Hili nipigo kubwa sana kwa nchi nalinaweza kuiingiza nchi
katka kulipa fidia ya mabillioni ya pesa ,iwapo Serikali haitaliangalia kwa
makini,hasa katika kuakikisha inakata rufaa.
Tanzania imetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi zinazo-ongoza kwa
rushwa Mahakama za Tanzania ni miongoni
mwa taasisi zinazo ongoza kwa rushwa kitu kinacho punguza nguvu mapambano zidi
ya madawa ya kulevya,ujangili nchini,rushwa ya waziwzi inafanyika na hakuna
juhudi zozote zinazofanyika kuzuia hali hiyo.
Rais Kikwete amekuwa analalamikia kushamili kwa rushwa nchini
kuanzia mahospitalini mahakama polisi
tra hakuna chochote kinachofanyika kutokomeza rushwa nchini,hali ni mbaya sana
,Wachina wanaokamatwa kwa uhujumu uchumi wanapofikishwa mahakamani wanaachiwa
katika mazingila tata katika mahakama zetu chini ,wengine wanapigwa faini ndogo
sana ukilinganisha na makosa waliyofanya.Upande wa mashitaka wamekuwa
wanapeleka ushahidi afifu mahakamani kwa makusudi.
Baba wa Taifa amewahi kusema Tanzania inanuka rushwa.
