Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Maktaba ya
Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library) iliyo katika Taasisi ya
Bush (George W. Bush Institute) mjini Dallas, Texas, na kujionea nafasi
kubwa iliyotolewa kwa Tanzania na zawadi ambazo Rais Bush alizipata
katika ziara yake rasmi ya Tanzania wakati akiwa Rais wa Marekani.
Maktaba
hiyo ya kuvutia inaendeshwa kwa teknolojia ya kisasa kabisa ya habari
na mawasiliano. Rais Kikwete alikuwa amesimama mjini Dallas kwa muda
akiwa njiani kutoka Washington D.C., kwenda Houston, jimbo hilo hilo la
Texas kuhudhuria mkutano wa wafanyabiashara wa mafuta na gesi ambao
wanataka kuwekeza katika sekta hiyo katika Tanzania.
Rais
Kikwete amekuwa katika Marekani kwa ziara ya kikazi ya siku tisa,
ambako miongoni mwa mambo mengine, amehudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi
za Marekani na Afrika uliofikia kilele chake jana kwa kikao
kilichoendeshwa na Rais Barack Obama wa Marekani katika Wizara ya Mambo
ya Nje ya Marekani mjini Washington D.C.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (*Bush Presidential Library) sehemu ambayo imejengwa kwa mfano wa Ikulu ya Marekani, White House, hususan katika bustani ya Waziri (Rose Garden) pamoja na ofisi ya Rais wa Marekani, Oval office*
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea
na kujionea vitu mbalimbali ambavyo Rais mstaafu George W. Bush alipewa
kama zawadi kutoka Tanzania ambavyo vimehifadhiwa katika Maktaba ya Kirais
ya Rais Bush (*Bush Presidential Library) *
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea na kujionea vitu mbalimbali ambavyo Rais mstaafu George W. Bush alipewa kama zawadi kutoka Tanzania ambavyo vimehifadhiwa katika Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (*Bush Presidential Library) *

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiondoka baada ya kutembelea Maktaba
ya Rais ya Rais Bush (*Bush Presidential Library)
PICHA NA IKULU