Mkuu
wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro amepiga Marufuku malori kuwalaza
abiria katika magari barabara kutoka namkukwe kwemda Mbeya na Isangawana
kwenda Mbeya .
Ameyasema
hayo wakati wa Ziara ya kukagua ujenzi wa Mahabara katika Kata 20 za
Wilaya ya Chunya baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa
Namkukwe na Isanzu ambao wamedai kwamba magari huanza safari saa kumi na
mbili jioni na kupumzika katika kituo cha malangali kwa zaidi ya masaa
saba huku abiria wakiwa katika malori hayo.
Amewaagiza
maaskari kuyakamata magari yote yatakayokaidi Amri hiyo kutokana na
adha kubwa wanayopata wasafiri wanaotumia malori hayo.
Na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu