Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kesho Jumamosi (Septemba 13 mwaka huu) saa 4 asubuhi
litaendesha mafunzo ya matumizi ya tiketi za elektroniki kwa wadau wa
mpira wa miguu Dar es Salaam.
Mafunzo hayo Uwanja wa Taifa, na
kushirikisha wasimamizi wa mechi, viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na makatibu na maofisa habari wa klabu za
Azam na Yanga.
Washiriki wengine wa mafunzo hayo
ni Meneja wa Uwanja wa Taifa na msaidizi wake, wasimamizi wa milangoni
(stewards), waandishi wa habari wa Dar es Salaam maofisa usalama wa TFF.
Mafunzo hayo yatahitimishwa
Jumapili (Septemba 14 mwaka huu) kwa mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Azam
na Yanga kuanzia saa 10 kamili jioni. Tiketi zimeanza kuuzwa jana
(Alhamisi) kupitia M-Pesa, CRDB Simbanking na maduka ya Fahari Huduma.
BONIFACE WAMBURA
MKURUGENZI WA MASHINDANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)