Na Bernard James
+255 752106535
…………………………….
Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe:Lazaro Nyalandu akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam, alisema majangili hawana nafasi tena ,na
hawana pa kukanyaga katika nchi za Afrika mashariki na watanaswa
wote,aliyaongea hayo wakati wa mkutano wa wadau wa kimataifa na Serikali
waliokutana kuweka mikakati yanamna ya
kuzuia ujangili wa wanyamapori na hasa Tembo, ambao wapo hatarini kutoweka
kutokana na majangili kuwawindana
kuwaua kwa ajili ya kuchukua meno yao, ambayo yana soko kubwa katika nchi za
Mashariki ya mbali hasa China na Vietinamu,
Tanzania imefanya kila juhudi ya
kuutokomeza ujangili ,rakini jitihada hizo haziwezi kufanikiwa bila waTanzania
wote wenye mapenzi mema kushilikiana pamoja, Wizara ya maliasili pekee haiwezi
kumaliza tatizo hili bila kuunganisha nguvu zetu pamaoja, nakuanzia sasa baadhi
ya Wizara zitashilikiana na Wizara ya maliasili katika kuunda kikosi
kazi,ikiwemo Wizara ya Mambo ya ndani,Wizara ya Uchukuzi na Wizara ya Maliasili
na utalii yenyewe.
Pia Nyalandu alisema Wizara
imeanzisha mamlaka ya Wanyamapori na,
itajenganyumba za wafanyakazi na Morogoro ndio itakuwa makao makuu ya
mamlaka ya wanyamapori (TAWA) ambayo
wafanyakazi 70% kuhamia baada ya majengo kukamilika.
Mkutano huo wa wadau wa Kimataifa na
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili ulifanyika siku mbili 2 katika Hotel ya
Kimataifa yaHyatt Regency,ambao uliandaliwa na The ICCF Group
Waziri Nyalandu ambae ni mwiba mkari
kwa majangili nchini ,Majangili
wamejiunga kwa pamoja nakuweka mikakati ya kumkwamisha Nyalandu katika jitihada
zake za kuutokomeza ujangili,mikakati hiyo inalatibiwa na aliyewahi kuwa Waziri
katika Wizara hiyo ya maliasili akishilikiana na baadhi ya wafanyabiashara ya
utalii na wamiliki wa baadhi ya vitalu vya uwindaji,walengwa wakubwa katika
mikakati hiyo ni Mhe,Lembeli,Nyalandu,na Sarakikya ambae ni kaimu mkurugenzi wa
Wanyamapori,mikakati hiyo nipimoja nakutolewa kwenye magazeti kurasa za mbele
kila wiki ,kwakuwabambikizia tuhuma mbalimbali,ikiwemo Nyalandu kumihusisha na
ujangili na CIA na Uraia wa Marekani,mikakati hiyo lengo lake kumfanya Mhe Rais
wa Jamhuri ya Muungano kumuondoa katika nafasi hiyo. Baadhi ya wamiliki wa vitalu nchini na
baadhi ya wenye makampuni ya Utalii nchini wamekuwa wakihusishwa katika
ujangili wa Tembo na wanyama wengine,hutumia mwanya wa kukata vibari vya
wanyama kwa idadi furani,rakini wakifika porini wanauwa wanyama zaidi ya idadi
waliyolipia,Baadhi ya majangili wamebuni mbinu mpya wameweza kujipenyeza mpaka
kwenye jumuiya za wanavijiji wanaopakana na mbuga za wanyama ,mpori ya akiba,na
tengefu na kuwawafazirili wa jumuiya
hizo ilikuficha madhambi yao,pia wameweza kujipenyeza mpaka kwenye chama cha
mapinduzi ccm nakuwa viongozi,na
wafadhili,hii yote katika kuficha makucha ,yao kitu ambacho ni hatali kwa
ustawi wa malisili zetu ,tukidanganyika nao na ufadhili uchwara wao.
pia Nyalandu alitangaza kufanyika kwa
mkutano mkubwa nchini Nov 7-8-2014 utakao kutanisha maTaifa majilani zetu Nchi za Malawi, Zambia, Uganda
Msumbiji ,Mkutano huo utajadili mauaji ya Tembo kwa nchi hizo na namna ya kudhibiti majangili ambao uhamahama pindi
wanapofanya uhalifu na kukimbilia nchi moja wapo,maana majangili wanafahamiana
nikama wafanya biashara ya madawa ya kulevya,pia viongozi wa Dini
watashirikishwa aliongeza Nyalandu,na tarehe4/11/2014 utafanyika mkutno
mwingine wa ki-Mataifa kujadili ujangili,ambao bado haujaisha.
Katika mkutano huu uliomalizika
alhamis 9/9-2014 Wadau mbalimbali wa kimataifa walishiriki wakiwemo ma-barozi
mbalimbali na mashirika ya kifedha na Taasisi
Barozi wa China Mr Lu Youging
aliahidi nchi yake kutoa msaada wa vitendea kazi yakiwemo magari,pia china
itatoa mafunzo na ushauli mbalimbali kwa Tanzania Barozi Lu alisema China
inauzoefu wa miaka40 wakukabiliana na ujangili nchini mwao ,ambapo wanyama aina
ya Panda na Tiga walikuwa wapo hatalini kutoweka China, rakini China iliweza
kuidhibiti hali ya ujangili na kila jangili aliyekamatwa alipewa adhabu kali
,kitu kilichopelekea kukomesha ujangili,pia Lu aliahidi kuyayashauli makampuni
ya china yaliyopo nchini kusaidia kutoa misaada mbalimbali
itakayohitajika,makampuni hayo ni yale ya ujenzi na Huawei,pia atayashauli
makampuni ya China yaje kuwekeza katika
utalii nchini ilikuongeza pato lamtu masikini na kuwa mtu mwenye kipato cha
wastani kitu kitakachowafanya
wasiji-ingize katika ushawishi wakufanya ujangili ,
Nae
mbunge wa Iringa ambae pia ni Waziri Kivuli wa Maliasili kambi ya
upinzani ,Aliipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii katika jitihada zake kubwa
za kuhakikisha ujangili unatoweka nchini,mapambano dhidi ya ujangili sio ya
Nyalandu,ccm,cuf wala chadema bali ni ya kila M Tanzania,hii ni vita kama ile
ya kumuondoa nduli Idi Amini wa Uganda ambapo waTanzania wote tuliungana katika
kumpiga Nduli,kambi ya upinzani inapongeza jitihada zote zinazofanywa na
Nyalandu kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali.aliviomba vyombo vya habari
nchini kuunga mkono jitihada hizo zinazofanywa na Serikali kwa kuandika mambo
ya ukweli na kutia nguvu kwa wale wote wanaofanya juhudi katika kutokomeza
ujangili ambayo Waziri ameonyesha kuzifanya na ziko wazi.
Msigwa aliongeza kwa kusema sasa
uzalendo uwe mbele kwa kila mTanzania ,haiwezekani yakaja majangili yakafanya
ujangili bila kushilikiana na WaTanzania wenyewe na ndio wanaowaonyesha njia
zote zakupitia katika kutekeleza ujangili huo alionya Msigwa.
