Random Posts

SHULE ZA ST MARY NA FILBERT BAY ZASHUKA KIELIMU NCHINI

Na Bernard James-+255752106535


Shule za St Mary zinazomilikiwa na Dr Mama Rwakatale na Filbert Bay zimeshuka kitaaluma hivyo kusababisha wazazi wanaosomesha watoto katika shule hizo kuwahamisha watoto wao katika shule nyingine imefahamika.
Tofauti na katika miaka ya 2000 ambapo kila mzazi aligombea nafasi katika shule hizo ili mtoto wake asome hapo,
Katika mahafali ya 13 ya kuwaaga wanafunzi wanaomaliza katika shule ya Filbert Bay,Mkurugenzi wa shule hizo na mmiliki Anna Bayi alitumia muda mwingi kuishutumu Serikali ya Dr Mrisho Kikwete,kwamba,Serikali kupitia wizara ya elimu haijafanya chochote katika kukuza elimu nchini,zaidi ya kuwalimbikizia kodi kila kukichakitu kinachosababisha kushindwa kutoa misaada kwa shule nyingine ,hasa za serikali ambazo hazina madawati, na vitabu,na kwamba hali ikiendelea hivyo baada ya miaka 5 kuanzia sasa elimu itakuwa taabani kuwahi kutokea na kutakuwa hakuna elimu katika shule za serikali ambazo wanaosoma ni wa toto wa wakulima na masikini, alisema Anna Bayi ,
Hata hivyo madai ya Anna Bayi yamepingwa na wadau mbalimbali walio-ongea na Mtazamomedia,nakuitetea serikali iliyopo madarakani,  kwamba, inafanya kila jitihada mbalimbali kuakikisha elimu inapanda na kuboreshwa ,Mhe Rais Kikwete ametoa agizo kwa kila shule za Serikali nchi nzima ifikapo  desemba 30 /2014 ziwe zina-maabara, hili ni agizo a lilotoa mhe Rais kwa manisipaa zote nchini ,na hili agizo limeisha anza kutekelezwa na manisipaa nyingi nchini,ikiwapo manisipaa ya kinondoni,ambayo hivi karibuni iliitisha kiakao na kukutana na wadau mbalimbali wa elimu kujadili namna ya kupata pesa zitakazo wezesha kujengwa kwa maabara ili wanafunzi waweze kupata elimu kwa njia ya nadharia na vitendo,kitu ambacho ni hatua muhimu sana katika kufikia upatikanaji wa elimu bora nchini.
Imezuka tabia kwa baadhi ya watu na taasisi mbalimbali kubeza kila kitu kinachofanywa na Serikali,ama kiwe kizuli au kinakasoro,Serikali ya awamu ya4 imefanya mambo mengi mazuli rakini baadhi ya watu kwa makusudi wamekuwa wanabeza kama vile hawaoni alisema Mzee Athumani wa Magomeni Usalama,