![]() |
| SAMSON Simkoko Diwani kata ya Halungu aliyeibua tuhuma za Mkuu wa wilaya ya Mbozi |
![]() |
| DC MBOZI DKT Kadeghe anayetuhumiwa kuwalambisha mshiko wanahabari |
Septemba
5 Mwishoni wa wiki iliyopita kulikuwa na taarifa za baadhi ya waandishi
wa habari kulambishwa mshiko (Rushwa) kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya
Mbozi Dkt. Michael Kadeghe kwa kile kilichoelezwa kuzuia kutolewa kwa
stori inayomhusu juu yua ubadhirifu wa fedha za Halmashauri ya wilaya ya
Mbozi.
Tuhuma
hizo kwa waandishi wa habari ziliibuka baada ya baadhi ya waandishi wa
habari kutuma stori hiyo News Room ambako walitakiwa kubalance kwa Mkuu
huyo ili kumpa nafasi ya kujieleza kutokana na tuhuma alizokuwa
akikabiliwa nazo.
Kwa
mujibu wa maelezo ya tukio hilo ni kuwa baada ya kumalizika kwa kikao
ambacho madiwani wa Halmashauri hiyo walimshambulia wazi wazi Mkuu huyo
wa wilaya kwa kile kilichoelezwa kuwa ni miongoni mwa waliosababisha
kupatikana kwa hati ya Mashaka kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
Ilikuwa
ni katika kikao cha kupitia Hoja za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
kwa mwaka 2013-2014 ambapo takribani hoja 100 zilikuwa bado hazijafungwa
na hivyo kuonesha namna ambavyo Halmashauri hiyo imeshindwa kuwajibika
vyema katika ukusanyaji wa mapato.
Ilielezwa
kuwa mara baada ya kumalizika kwa kikao mmoja waandishi wa Habari(jina
tunalo) alikutana na Mkuu huyo wa Wilaya ambapo ilielezwa kuwa
alitengeneza ushawishi wa kukubaliana na Mkuu huyo wa Wilaya ili
kumsaidia kupunguza makali ya taarifa itakayotolewa kwenye vyombo vya
habari.
‘’Yule
mwandishi tulimuona yuko pembeni wanateta na Mkuu wa wilaya
wakizungumza kilugha ( Lugha ya asili) wakazungumza kwa muda mrefu
walionesha kukubaliana jambo’’ alisema mmoja wa watoaji wa taarifa hizi
aliyekuwa akifuatilia kikao hicho.
Inadaiwa
kuwa mara baada ya makubaliano mwandishi alimweleza DC kuwa yeye anao
uwezo wa kuwashawishi waandishi wenzie kutotoa stori hiyo hivyo ampe
mshiko ambao atawagawia wenzie, DC inadaiwa akakata mshiko wa kutosha
ambao hadi sasa haujulikani ni kiasi gani.
Wakati
wanahabari wakiwa wanarejea Mbeya kutokea Mbozi, walikuwa katika
majadiliano juu ya stori hiyo huku wakielezea namna ambavyo DC huyo
alivyoshambuliwa na Madiwani na kuwa kitendo hicho ni ukiukwaji wa
maadili ya Uongozi.
Katika
mjadala huo inaelezwa kuwa mwandishi anayedaiwa kulamba mshiko alikuwa
amenyamaza kimya huku akichombeza maneno machache ya kuwashawishi
waandishi wajaribu kumuonea huruma mkuu huyo kwa kutoandika habari kali.
Hata
hivyo inaelezwa kuwa alipoonm msimamo wa waandishi hao juu ya kuandika
stori hiyo, kesho ya Septemba 6 asubuhi aliwapigia baadhi ya waandishi
na kuwaeleza kuwa amepewa hela na Mkuu wa wilaya ili isiandikwe stori
hiyo.
Baadhi
ya waandishi(majina tunayo) walikiri kupigiwa simu na mwandishi huyo na
kudai kuwa alipewa fedha kiasi cha shilimgi Laki moja( 100,000) ili
awagawie waandishi wa habari kila mmoja elfu ishirini(20,000) kati ya
waandishi watano na kuwa waandishi wengine watano waliobaki stori zao
hazina impact kubwa hata kama wataandika.
Mmoja
wa waandishi ambaye aliandika stori yake na kuituma News Room kwake
alipigiwa simu na Mhariri wake kwamba anapaswa kuibalance stori hiyo kwa
Mkuu wa wilaya ambaye ametuhumiwa na Madiwani, alipompigia DC huyo ili
kuibalance alidai kuwa Mkuu huyo alimuuliza kama hajawasilana na wenzie.
‘’Nilipompigia ili kuibalance alishangaa na kuniuliza vipi Bwana Mdogo hujawasiliana na ……. ?(alitaja jina la mwandishi aliyepewa mshiko ili awagawie wenzie).
‘’Mie
nilishituka sana kuambiwa huyu..(alitaja jina la Mwandishi) kuwa
amelamba mshiko halafu amekaa kimya bila kuwaeleza wenzie,lakini hata
hivyo DC ni mtu mmoja na Madiwani ni wengi wanawawakilisha wananchi
wapatao laki nne, kumbeba DC na kuwatosa wananchi wengi sio fare
kabisa,’’alisema Mwandishi huyo.
Septemba 7 ikiwa imepita siku
mbili baada tukio hilo mwandishi wa Blogu hii alipigiwa simu na
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi, Elick Ambakisye na
kuelezea masikitiko yake juu ya kitendo kilichofanywa na waandishi wa
habari kula rushwa.
Ambakisye
alielekeza lawama zake moja kwa moja kwa waandishi huku akitaja jina la
Mwandishi aliyedaiwa kushikishwa MSHIKO na DC na kusema kuwa kikao
kizima cha Halmashauri ya Chama kiliwatupia lawama waandishi na kudai
kuwa upo ukweli wa jambo hilo kwa kuwa hakuna chombo hata kimoja
kilichotoa stori ya kikao hicho.
Aidha
Ambakisye alisema kuwa hata hivyo kikao hicho hakikumalizika salama
kutokana na taharuki iliyokuwepo kati ya Madiwani na DC na kuahirishwa
hadi siku ya pili.
Septemba 8 Mwanablogu
wetu alitinga wilayani humo na kukuta kikao kikiendelea ambacho
kilikuwa na mvutano mkubwa kati ya Uongozi wa CCM wilaya na Madiwani wa
Halmashauri hiyo wakiwemo watendaji wa Halmashauri ya wilaya, kikao
hicho kilifanyika katika ukumbi wa chama wilaya.
Kikao
hicho kilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa CCM mkoa ambaye ni Mbunge wa
Jimbo la Mbozi Mashariki Godfrey Zambi ambapo hatima ya kikao hicho
ambacho kiliwashutumu Madiwani kutowajibika vyema katika kuwasimamia
watendaji wa Halmashauri hiyo, ilipendekezwa wajiuzuru nafasi zao.
Wakiwa
nje mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa George Mwenisongole alitoka
nje ya kuwaeleza wanahabari kuwa baadaa ya kikao hicho atakuwa na maneno
ya kuzungumza na waandishi ambapo pia alitoa tahadhari kwa kusema kuwa
lakini wasifanye kama alivyofanya mwandishi( alimtaja jina) aliyechukua
mshiko kwa DC.
‘’Nitaongea
nanyi baada ya kikao ila msifanye kama mwenzenu(alimtaja jina)
amechukua habari then akaenda kulamba mshiko kwa DC hiyo sio fare ndugu
zangu tunawategemea kama kioo cha jamii na kisemeo cha
wanyonge,’’alisema Mwenisongole.
Mara
baada ya kumalizika kwa kikao hicho nje ya ukumbi Mkuu wa Wilaya
alipotoka na kuonana uso kwa uso na Waandishi wa Habari alionesha
dhahiri kuwalaumu kutokana na Stori iliyosoma kwenye moja ya Televisheni
mchana wa siku hiyo
‘’
Mmenidhalilisha sana pamoja na kujipendekeza kwangu kwenu, lakini
mmetoa ile habari mme ni –demoralized sana okay mmeamua kuitoa hiyo
stori yaani pamoja na kujiwekea urafiki na ninyi mmeamua kunifanyia
hivyo? alilalamika Dkt.Kadeghe mbele ya waandishi wachache waliokuwepo
nje ya ukumbi wa CCM wilayani humo.
Hata
hivyo taarifa za kupewa mshiko kwa waandishi na DC kumeelezwa ni tamaa
ya waandishi hao iliyotokana na ukata na kuwa inaelezwa kuwa Mwandishi
aliyekula mshiko alifanya hivyo kwa nia ya kujiongezea kipato kwa njia
zisizo halali na hivyo kuweka pembeni taaluma yake kwa kujinufaisha.
Mwanablogu
wetu hakuishia hapo alim -face moja kwa moja mwandishi aliyetuhumiwa
kulamba MSHIKO kutoka kwa DC kwa nia ya kuzima soo yake, Mwandishi huyo
pamoja na kutajwa wazi wazi kuhusika na sakata hilo alikanusha macho
makavu na kudai kuwa yeye hawezi kufanya jambo hilo.
MWANABLOGU: Lakini unadaiwa kuhusika moja kwa moja na skendo hii na umetajwa jina lako,unasemaje kuhusu suala hilo.
MWANDISHI: Hayo ni
majungu tu, mie sijahusika kabisa, tena kule kuna stori nyingi sana
ukiacha hiyo skendo mie nikiamua nitaandika mabaya zaidi ya hayo.
MWANABLOGU: Lakini unaelezwa kuwa ulikuwa umekaa pembeni unazungumza kilugha na DC umesikika na watu wamekuona, hilo unalizungumziaje.
MWANDISHI: Pale
niliposimama tulikuwa mimi, DC na Mkuu wa Mkoa Mzee Kandoro, hatukuwa
na nafasi ya kuteta kwa lugha yoyote pale nilikuwa Napata ufafanuzi juu
ya kikao kile lakini si hayo unayoniuliza.
MWANABLOGU: Inadaiwa
kuwa mmelamba mshiko na Stori hamjaandika,unaweza kunieleza kwanini
hamkuandika stori kubwa na yenye hisia za kijamii kama ile, kutoandika
kwa stori hauoni kuwa itahalalisha kuwa mmelamba mshiko?
MWANDISHI: Mie
nilichelewa kutuma stori yangu, wala si kwa ajili ya kulamba mshiko,
potelea mbali kama nitaeleweka vinginevyo, stori hazipo Mbozi pekee yake
ninaweza kwenda kufanya katika wilaya nyingine, tena wana skendo nyingi
sana wale nikiamua kuandika wataumia sana.


