Random Posts

PAMBANO LA KARNE KUFANYIKA MAY 15-2015 KATI YA FLOYD DHIDI YA PACGUIAO

Marcos Maidana kulia akipokea ngumi ya jebu kutoka kwa Floyd Mayweather

IMEANDALIWA NA BERNARD KWA NIABA YA MTANDAO
 .
Pambano la karne la Ngumi kugombea mikanda ya uzito WBA –WBC na SUPERWELTER WEIGHT TITLE kufanyika May 15/2015 kati ya wapinzani wa kubwa katika uzani huo, kati ya Bingwa  wa Dunia,Floyd Mayweather,na Manny Pacguiao imefahamika jumamosi ,baada ya kumalizika pambano la kugombea ubingwa huo ,kati ya Floyd na Marcos Maidana lililofanyika septemba 13 -2014 na majaji wote 3 kumpa ushindi wa points Floyd,pambano hilo lilifanyika katika ukumbi wa Mgm Grand Garden ,Arena  Las Vegas,mala baada ya kutangazwa mshindi ,aliulizwa swali na waandishi wa habari kama yuko tayari sasa kupambana na Mfilipino Pacguiao ,alijibu milango iko wazi kwa kufanyika kwa pambano hilo ,ambalo linasubiliwa kwa hamu kubwa sana na wapenzi wa masumbwi Duniani.
Simuogopi wala kukwepa kupigana na Pacguiao tayari nimeongea na timu yangu nzima kuruhusu kufanyika kwa pambano hilo alisema Floyd alipokuwa akijibu maswali aliyoulizwa na waaandishi wa habari.
Iwapo hilo pambano litafanikiwa kufanyika ,wadau mbalimbali wa mchezo wa ndodi ,wamelitabilia kuvunja rekodi ya dunia litakuwa The super Ghost,na kila bondia litamuingizia kitita kikubwa cha dola,na litakuwa pambano lililodhaminiwa kwa pesa nyingi kuliko pambano lolote Duniani