Picha kwa Hisani ya Father Kidevu Blog
Mtandao wa www.mtazamomedia.blogspot.com, Tumepokea kwa masikitiko makubwa Taarifa za Ajali mbaya iliyotokea Musoma Ambayo ilihusisha Basi
la J4 Express T677CYC lililokuwa linatoka Sirari kwenda Mwanza
limegongana uso kwa uso na basi la Mwanza Coach T736AWJ Tarehe
5.09.2014 Majila ya Mchana katika eneo la sabasaba Musoma wakati moja ya
mabasi hayo likiovateki basi lengine ambapo watu zaidi ya 39
wamepoteza maisha huku wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa. Mpaka sasa Maiti
25 zimetambuliwa kati ya 39 na ndugu wa Marehemu.
Tunaungana
na watanzania wote kuwapa pole ndugu waliopotelewa na Ndugu, Jamaa na
Marafiki waliopoteza ndugu zao katika ajali hii, Pia tunawapa pole wale
Majeruhi wote Tunawaombea kwa Mungu wapate kupona Haraka ili tuje kuweza
kuungana nao katika Kujenga Taifa
