![]() |
| Baadhi ya wahitimu wa shule ya Filbert Bayi |
Bango likionyesha shule ya Filbert Bay iliyopo Kibaha kama ilivyokutwa na mpiga picha wetu September 6, 2014 wakati wa mahafari ya13 kwa upande wa shule ya msingi na mahafari ya 6 kwa upande wa secondari.
HABARI/PICHA NA BERNARD JAMES
0652152000
0652152000
.....................................................................
Mmiliki wa Shule za Filbert Bayi na Mkurugenzi,Bi. Anna Bayi akizungumza na baadhi ya waandishi (hawapo pichani), wakakati wa mahafari hayo.
Shule ya filberti bayi imefanya mahafari ya kuwaaga wanafunzi wanaomaliza shule hiyo mwaka huu.haya ni mahafari ya 13 kwa upande wa wanaomaliza darasa la7,pia ni mahafari ya 6 kwa wanaohitimu secondari.
Kwa upande wa Secondari Filbert Bayi haijawahi kutoa mwanafunzi aliyepata alama ya sifuli na mwaka jana hakuna mwanafunzi aliyepata alama 4 yaani division four,wengi walipata alama ya pili na kwanza na daraja la tatu.
na ilishika nafasi ya sita kimkoa kati ya shule 105 ambapo kitaifa ilikuwa ya71 kati ya shule zaidi ya3000.Shule ya Filbert Bayi inalichukulia umuhimu suala la michezo pia ili kuwaweka wanafunzi katika afya bora,imeweza kujenga viwanja vya aina mbalimbali vya michezo vyenye kiwango cha juu na nishule inayo ongoza kimichezo na stadi zingingine za kimaisha.
Shule pia imeweza kuanzisha mafunzo ya ujasiliamari kwa wanafunzi ,ili kuwaandaa wamalizapo masomo waweze kujitegemea ,na imeweka mafunzo aina tofauti,yapo mafunzo ya kuandaa bustani za mbogamboga,
kufuga kuku wa nyama na mayai,
usukaji na mapambo(saloon)ya aina mbalimbali mfano kupamba kumbi za sheehe majumba ya mikutano na kumbi za harusi ikiwemo kumuandaa bibi harusi.
Hii yote ni kumuandaa mwanafunzi anapo maliza masomo yake katika shule za Filbert Bayi asiwe mzigo kwa familia anakotoka ,awe na kitu cha kufanya alibainisha mama Bayi.
Kwa upande wa shule za msingi inawanafunzi 860 na ufaulu wake ni 100% na wanaomaliza nakufanyiwa mahafari leo ni 89 ambapo kwa upande wa sekondari ni38.
Kwa upande wa Elimu nchini
Anna Bayi anaomba Wizara husika isifanye sanaa katika Elimu nchini .Shule za serikali ziko hoi ,Shule za kata zinasononesha sana nyingi hazina maabara,vitabu madarasa ya kutosha walimu,vitabu vyoo,unakuta shule darasa moja linawafunzi160 aliitolea mfano shule moja iliyopo kibaha ambayo wdarasa moja linawafunzi 160 wanaokaa chini .Mtazamomedia imepanga itembelee shule hiyo ilikuweza kuiabalisha jamii wajue hali halisi,Mama Bayi ni mwenyekiti wa mfuko wa maendeleo wa shule kibaha.
Upande wa changamoto walizokutana nazo na zinazoendelea kuikabili shule ya Filbert Bayi kwa ujumla wake.Anna Bayi alitoa kilio chake kwa Serikali hasa jinsi wanavyotozwa kodi nyingi kila kukicha,Bayi anaiomba serikali kuwaondolea kodi shule binafisi kama walivyofanya kwa shule za dini,alitolea mfano shule za Filbert Bayi ada yake kwa mwaka milioni mbili 2 ni ada rahisi kabisa ukilinganisha ni huduma wanayoitoa kwa mwanafunzi,hata hizo shule zilizopewa msamaha wa kodi ada zao ni kubwa ,inakatisha tamaa sana,
Alitolea mifano wa kodi wanazolipishwa ikiwemo SLB yaani Service development Labour
ukaguzi 500 kwa kila kichwa
ukaguzi wa zima moto milioni2 kila mwaka
TRA ukaguzi kwa mwaka milioni2 na kodi nyingine nyingi zinabuniwa kila kukicha ilikuwaumiza aliseama mama Bayi kwa masikitiko..
Anna Bayi alisema angependa kutoa misaada kwa shule za kata rakini anashindwa kutokana na kodi kubwa anazolipishwa.
Habari zaidi kuhusu alicho-ongea mama Anna Bayi kuhusu watendaji wa Serikali na hatima ya elimu ya Tanzania ndani ya miaka5 ijayo tutairusha hivi karibuni.

.jpg)
.jpg)