Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea
James Rugemalira akizungumza na waandishi wa habari pamoja na jopo la
wanasheria kutoka Marekani (hawapo pichani kuhusu jambo hilo Dar es
Salaam leo. Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
Mwanasheria maarufu kutoka Amterdam
Holand, Dk. Camilo Schutte (kushoto), akitoa ufafanuzi wa kisheria
kuhusu jambo hilo. Kulia ni Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya VIP na
Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Joe Mgaya na Mshauri wa Kimataifa
wa Kujitegemea, James Rugemalira.
Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya VIP na Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Joe Mgaya.
Mwanasheria Respicius Didace akizungumza katika mkutano huo.
Dk. Isaya Tosiri, akizungumza katika mkutano huo.
Ofisa Fedha na Ugavi, Terevael Masawe akizungumza katika mkutano huo.
Mwandisi Mwandamizi wa Gazeti la Serikali Daily News, Faustine Kapama akiuliza swali kwa jopo hilo la wanasheria.
Justus Selestine kutoa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), akizungumza katika mkutano huo.
Mwanahabri akichangia hoja.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
Mgeni mualikwa Lise Heide kulia akifurahia jambo Evelyn Rugemalira katika mkutano huo.
Mwanasheria
maarufu kutoka Amsterdam Holand, Dk. Camilo Schutte (kulia), akiteta
jambo na Wakili Okare Joshua (kushoto) na Mshauri wa Kimataifa wa
Kujitegemea, James Rugemalira.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Benedicta Rugemalira (wa pili kushoto), akiteta jambo na wageni waalikwa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Benedicta Rugemalira (wa pili kushoto), akiteta jambo na Mwanasheria maarufu kutoka Amterdam Holand, Dk. Camilo Schutte.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitemea, James Rugemalira (kushoto) akizungumza katika mkutano huo.
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye mkutano huo.
Wageni kutoka Marekani wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwanasheria maarufu kutoka Amterdam Holand, Dk. Camilo Schutte akizungumza katika mkutano huo.
Mwanasheria Respicius Didace akiwa amepozi na mke wangu katika mkutano huo.
Mwanasheria maarufu kutoka Amterdam Holand, Dk. Camilo Schutte (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
KAMPUNI YA VIP YAOMBA TAKUKURU KUTOA TAARIFA DHIDI YA MADAI YA MBUNGE KAFULILA
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya VIP Engineering and Marketing
Limited imetoa wito kwa Mkaguzi Mkuu wa Serikari (CAG) na taasisi ya
kupambana na kuzuia rushwa (TAKUKURU) kutoa mapema taarifa ya uchunguzi
inayohusiana na uchotwaji wa fedha katika akaunti maalumu ya Escrow
Benki Kuu ya Tanzania.
Mwito huo umetolewa na Mshauri ya
Kimataifa wa Kujitegemea James Rugemalira wakati akiongea na waandishi
wa habari pamoja na jopo la wanasheria wa kimataifa kutoka Marekani
waliopo nchini Dar es Salaam jana kwa ziara maalumu.
“Mimi nashangaa kwa nini taarifa hizi
hazitoki. Nilitegemea zitoke hata jana. Mimi nimeshatoa maelezo yangu na
niko muwazi kwa jambo hili. Nilitegemea taarifa hizi ziwe zimeshatolewa
ili wananchi wajue ukweli wa swala hili,” alisema Rugemalira.
Rugemalira alisisitiza kuwa fedha zote
zilizowekwa kwenye akaunti hiyo si mali ya serikali na kwamba kampuni
yake iliuza kihalali hisa zake kwa kampuni ya Pan African Power
Solutions ambayo inawajibika kwa mujibu wa amri ya Mahakama Kuu kulipa
wadai wote wa kampuni ya IPTL.
Akizungumza na waandishi wa habari,
wakiri maarufu kutoka Uhi, Dk Camilo Schutte, aliishauri serikali ya
Tanzania kuwaeleza ukweli wahisani na wafadhili hapa nchini kuwa fedha
zinazobishaniwa si mali ya umma bali ni fedha zinazohusu makampuni
binafsi.
Wakili huyo alisikitishwa na kitendo cha
wafadhili hao kusitisha ufadhili wa kuunga mkono bajeti ya serikali ya
Tanzania kwa kusikiliza maneno ya pembeni kuwa fedha zinazobishaniwa ni
mali nya umma. “Seriklali iwaambie watanzanmia ukweli.
Hizi sio fedha za umma . Ni mali inayohusu makampuni binafsi,” alisisitiza.


0 Comments