Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akifungua Mkutano wa
Kamati Kuu ya CCM kwenye Ofisi Ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar
es salaam Juni 18, 26. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip
Mangula na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM , Abdulrahman Kinana.
Makamu wa Rais Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi wakifuatilia kikao cha
Kamati Kuu ya CCM kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu
Jakaya Kikwete kwenye Ofisi ndogo ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es
salaam Juni 18, 2016.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete wakati alipofungua kikao chao kwenye Ofisi
ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam Juni 18, 2016.
(Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)



