Wakufunzi wa mafunzo ya Uongozi kutoka Chuo cha Uongozi Institute Dkt. Jochen
Lohmeier (kushoto) na Nathaniel Mjema wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza
mafunzo ya siku tatu kwa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wa Serikali ya
Zanzibar yaliyofanyika katika Ofisi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Maisara
Mjini Zanzibar.
Mkufunzi Nathaniel Mjema akiwasilisha mada ya kujitathmini kwa viongozi wanaoshiriki mafunzo
ya uongozi yaliyowashirikisha Makatibu wakuu na wasaidizi wao.
Waratibu wa Mafunzo hayo wakifuatilia kwa kina uwashilishwaji wa mada mbali
mbali zilizowasilishwa katika mafunzo hayo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid
Salum akitoa mchango katika mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya Maendeleo endelevu yaliyowashirikisha Makatibu
Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu wa Serikali ya Zanzibar.
Dkt. Jochen Lohmeier kutoka Uongozi Institute akitoa mada kuhusu kuitathmini
Jamii katika mafunzo ya Makatibu wakuu na Wasaidizi wao yanayofanyika Ofisi ya
CAG Maisara, Mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Ali Khalil Mirza (kulia)
na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Juma Ali Juma
wakinakili mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakibadilishana mawazo na kujadiliana kutokana na
kazi waliyopewa na wakufunzi wao.
Picha na Makame
Mshenga/Maelezo Zanzibar.






