Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na mamia
ya wananchi wa Kijiji cha Nyakabale, Kata ya Mgusu, mkoani Geita ambao ni
majirani wa Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ya GGM mkoani humo. Wananchi hao
wamelalamika kuwepo na vitendo vya ukatili dhidi yao vinavyofanywa na baadhi wa
askari wa kampuni hiyo. Hata hivyo Mhandisi Masauni aliwataka Polisi mkoani humo
kufanya uchunguzi wa haraka dhidi ya tuhuma hizo.
Mkazi
wa Kijiji cha Nyakabale, Kata ya Mgusu, mkoani Geita, Biosi Makongoro akitoa
kero yake kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(kushoto aliyekaa) dhidi ya Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ya GGM mkoani humo
ambayo ipo jirani na kijiji hicho, kuwa askari wa kampuni hiyo wanadaiwa
kuwanyanyasa wananchi hao wanapopita katika eneo la Kampuni hiyo. Hata hivyo
Mhandisi Masauni aliwataka Polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa haraka dhidi
ya tuhuma hizo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiwasili
Kituo cha Polisi Runzewe kilichopo Kata ya Uyovu wilayani Bukombe ambacho
Mbunge wa Jimbo hilo, Dotto Biteko aliuliza swali la nyongeza Bungeni hivi
karibuni akisema kituo hicho kinahitaji matengenezo makubwa na kumuomba Naibu Waziri
huyo kufanya ziara jimboni kwake kujionea kituo hicho. Hata hivyo, Masauni
alisema Serikali yake itahakikisha kituo hicho kitakuwa katika hali nzuri.
Mkuu
wa Kituo cha Polisi Runzewe kilichopo Kata ya Uyovu wilayani Bukombe, Jackson Kirahuka
akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto
aliyevaa koti) sehemu mbalimbali za kituo hicho ambacho Mbunge wa Jimbo la
Bukombe, Dotto Biteko (katikati) aliuliza swali la nyongeza Bungeni hivi
karibuni akisema kituo hicho kinahitaji matengenezo makubwa na kumuomba Naibu
Waziri huyo kufanya ziara jimboni kwake kujionea kituo hicho. Hata hivyo,
Masauni alisema Serikali yake itahakikisha kituo hicho kitakuwa katika hali
nzuri. Aliyevaa Kaunda suti ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Amani Mwenegoha.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kushoto) akizungumza
jambo na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali, Mstaafu Ezekiel Kyunga (meza
kuu), Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Msukuma (kulia), na Mkuu wa
Jeshi la Polisi mkoani humo, Mponjoli Mwabulambo, wakati Naibu Waziri huyo
alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimfafanulia jambo Mbunge
wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Msukuma (watatu kulia), na Mkuu wa Jeshi la
Polisi mkoani humo, Mponjoli Mwabulambo (wapili kushoto), wakati Naibu Waziri huyo
alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akitoka ofisi
ya Mkuu wa Wilaya ya Bukendo, Amani Mwenegoha (kushoto) mara baada ya kumaliza
kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo iliyopo mkoani Geita. Naibu
Waziri alifanya ziara ya kikazi mkoani Geita.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.






