Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, akizungumza na watumishi kabla yakupokea msaada wa gari la wagonjwa.
Balozi,
Issaya Chialo, alipokuwa akitoa maelezo mafupi juu ya msaada wa gari la
wagonjwa walilo likabidhi kwa hospitali ya Mkoa wa Mwanza.
Mganga
mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Subi, akitoa maelezo ya awali kuhusu huduma
za afya katika mkoa wa Mwanza wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyamagana, Bi Maricella, akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Wananchi
wanao hudumiwa katika hospitali hiyo ya mkoa nao hawakuwa nyuma katika
hilo, hapo wakisiliza kwa makini maelezo ya mkuu wa mkoa.
Watumishi
katika hospitali ya Mkoa wa Mwanza, wakimasikiliza kwa makini mkuu wa
mkoa wa Mwanza hayupo pichani, wakati wa hafla fupi yakukabidhi gari
hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, akikabidhi cheti cha Shukrani kwa
Balozi Issaya Chialo, kama sehemu ya shukrani kwa kutambua mchango wa
Rafiki Surgical Mission, walio utoa kwa Mkoa huo wa Gari la
Wagonjwa.(Habari na picha zote na Afisa habari wa mkoa wa Mwanza)
Mkuu wa mkoa akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa mapokezi ya Gari la Wagonjwa kutoka Rafiki Surgical Mission.
Muonekano wa gari lililotolewa na Rafiki Surgical Mission.
.......................................................................................................
Na.
Atley Kuni RS Mwanza.
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza John Mongella amepokea gari la Wagonjwa kutoka kwa Sargical
Rafiki Mission kwaajili ya kuhudumia
wananchi wa mkoa huo ambalo amelikabidhi kwa uongozi wa hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekouture na
kuwataka kuitunza kwa maslahi mapana ya wananchi wa mkoa huo.
Akizungumza
kabla yakupokea gari hilo mkuu huyo wamkoa amesema, msaada walio upokea kutoka
kwa Rafiki Mission ni masaada wakupigiwa mfano kwakuwa watu wengi wanabarikiwa
vitu vingi lakini suala lakutoa misaada wameshindwa.
Mongella
amesema kama mkoa ukipata marafiki wa aina ya Rafiki hawana budi kuwa ng’ang’ania
wasiondoke kwenye himaya yao. “ Nafahamu hata sisi tunabarikiwa sana lakini hata
siku moja hakuna mtu aliwahi kuleta hata mkasi, hivyo lazima tufahamu kutoa ni
moyo na sio utajiri.
Katika
hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa
amesema, karibu asilimia tisini ya matatizo ya afya yanayo ikabili jamii
ya kitanzania
yamejikita katika suala la afya ya mama na mtoto ambayo kama taifa
tukifanikiwa kuwekeza katika hili, basi matatizo mengine ya afya
yataondoka yenyewe “ Najua suala
la mama na mtoto ni tatizo mtambuka kwa taifa, hivyo tukiwekeza zaidi
katika
afya ya mama na mtoto tutakuwa tumekabili changamoto kubwa ya masuala ya
afya na itawawezesha wananchi kujikita katika shughuli za maendeleo”,
alisema Mongella
Awali
akitoa salama za Rafiki Mission, Balozi Issaya Chialo, alisema wao kama Rafiki
Mission, wanatambua matatizo yanayo ikabili jamii ya kitanzania hususan masuala
ya afya, na kwamba wao kama Rafiki Surgical
mission, hawana ubaguzi katika utoaji wa misaada kwa jamii nzima ya kitanzania.
“ Mkuu wa mkoa sisi shughuli zetu zipo katika mkoa wa Mtwara tukijikita katika
zaidi katika utafutaji wa mafuta na Gesi, lakini hiyo haituzuii sisi kupeleka misaada pembe
zingine za nchi na ndio maana leo tupo katika mkoa wako wa Mwanza” alisema Balozi
Chialo nakuongeza kuwa, wanajisikia fahari katika hilo.
Chialo
ameutaka uongozi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Seko’uture kulitunza gari hilo
la wagonjwa lenye thamani ya Mil. 40, ambalo litasaidi katika kuwakimbiza wagonjwa
wenye mahitaji maaluma sehemu mbali mbali za mkoa huo na mikoa ya jirani.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dkt. Subi, amesema hivi sasa
hospitali ya mkoa huo inakabiliwa na changamoto ya chumba cha kutolea huduma ya
upasuaji kwa akina mama, ambapo mkuu wa mkoa amemtaka Mganga huyo wa mkoa kutenga kiasi cha
Mil. 5 kutoka katika makusanyo ya ndani ya hospitali ya mkoa huo na Mkuu wa mkoa kupitia wadau wa
maendeleo atahakikisaha kiasi kingine cha fedha kinacho salia kinapatikana kwaajili ya
ukarabati wa chumba hicho ambacho kinahitaji Mil.20 ili kiweze kufanya kazi ya
upasuaji kwa akina mama.
Hospitali
ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Seko’uture,
imekuwa msaada kwa wagonjwa wa mkoa huo na mikoa ya jirani kutokana na huduma
zake kuwa nzuri na madaktari mabingwa wanaopatikana katika mkoa huo.








