Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkurugenzi Mkuu
wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt. Modestus Francis Kipilimba Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu
wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt. Modestus Francis Kipilimba akisaini mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini hati ya kiapo baada ya kumuapisha Mkurugenzi Mkuu
wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt. Modestus Francis Kipilimba Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu
wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt. Modestus Francis Kipilimba
...........................................................
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24
Agosti, 2016 amemuapisha Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu
wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Dkt.
Modestus Francis Kipilimba ameapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam na mara baada
ya kuapishwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa amekula kiapo
cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe.
Jaji Salome Kaganda.
Kabla
ya uteuzi huo Dkt. Kipilimba alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Dkt.
Modestus Francis Kipilimba amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Rashid
Othman ambaye amestaafu.
Aidha,
Rais Magufuli amemteua Bw. Robert Msalika Makungu kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania Bara.
Kabla
ya uteuzi huo Bw. Robert Msalika Makungu alikuwa Afisa Ubalozi katika Ubalozi
wa Tanzania nchini Ethiopia.
Wakati huo huo,
Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa
Taifa Bw. George Madafa kuwa Balozi na nchi atakayopangiwa itatajwa baadaye.
Wakurugenzi
na Naibu Wakurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa waliopo wanaendelea na nafasi
zao.



