Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiweka sahihi katika kitabu cha
wageni wakati wa ziara yake katika Vizuizi vya barabarani (Mizani) na Mipakani
kwa lengo la kufanya Tathimini ya Utekelezaji wa mpango wa maboresho ya
mazingira ya biashara na uwekezaji nchini Septemba 15, 2016.
Msimamizi wa Kituo cha
Mamlaka ya Mapato TRA kilichopo Mkoani Pwani Bw. David Kisanga akitoa maelezo
juu ya utendaji wa ofisi zao kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na
Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati alipotembelea ofisi hizo Mkoa wa Pwani.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akimsikiliza Msimamizi wa Kizuizi
cha Vigwaza Mkoani Pwani Bw. Titus Michael wakati wa ziara yake kujionea hali
halisi ya vituo hivyo kwaajili ya Maboresho ya mazingira ya biashara na Uwekezaji
nchini.
Baadhi ya magari yakipima
uzito wa mizigo katika Mizani ya Vigwaza mkoa wa Pwani, Septemba 15, 2016.
(Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)




0 Comments