Kaimu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (katikati) akitoa
hotuba ya kufunga mafunzo ya Usimamizi
na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika Sekta ya Umma kanda ya kati
iliyojumuisha mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara katika ukumbi wa VETA mjini
Dodoma. Kulia ni mkufunzi wa mafunzo hayo, dkt. John Mduma kutoka Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam na kushoto ni Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi
Jumla,Tume ya Mipango, dkt. Lorah Madete.
Washiriki wanaounda kundi la nne wakijadili maswali juu ya utayarishaji na
uchaguzi wa Miradi ya uwekezaji.
Washiriki kundi la kwanza wakijadili maswali waliyopewa na wakufunzi kabla ya kuhitimishwa kwa mafunzo hayo Septemba 16,
Washiriki
kundi la pili wakifanya maswali waliyopewa na wakufunzi mara baada ya kuhitimisha somo.
Washiriki kundi la tatu wakifanya
maswali kutoka kwa wakufunzi katika ukumbi wa VETA mjini Dodoma.
..................................................................................................................
Na Adili Mhina, Dodoma.
Tume ya
Mipango imehitimisha mafunzo ya Usimamizi na Utayarishaji wa
Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma yaliyowahusisha maofisa mipango
wa Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri kutoka Mikoa
ya Singida, Manyara na Dodoma yaliyofanyika tarehe 12-16 Septemba, 2016
katika
ukumbi wa VETA mjini Dodoma.
Akifunga mafunzo hayo Kaimu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango, Bibi
Florence Mwanri aliwasihi washiriki kutumia ujuzi waliyoupata katika kuandaa,
kutekeleza miradi ya Umma kwa njia za kisasa ili kuongeza ufanisi wa miradi na
kuharakisha maendeleo ya wananchi.
Alisema kuwa Tume ya Mipango imefanikiwa kutekeleza wajibu wake wa
kuwajengea uwezo maafisa hao katika hatua zote muhimu zinazopaswa kuzingatiwa
katika kufanya maandalizi, kutekeleza, kusimamia, kufuatilia na kufanya tahmini
ya miradi ya maendeleo.
“Ni matumaini yangu kuwa hizi siku tano hazijapotea, mmepata elimu ya kutosha
kutoka kwa wataalamu wetu katika masuala yote muhimu yanayohusu miradi ya Umma.
Jukumu mlilonalo kwa sasa ni kuhakikisha mnatumia mbinu mlizofundishwa katika
kutekeleza miradi ya serikali kwa usahihi ili tufikie malengo ya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano,”
Alisema.
Nao washiriki wa mafunzo hayo walieleza kuwa wamepata elimu muhimu ambayo
itarahisisha utendaji katika kusimamia miradi na kutoa ushauri wa kitaalamu
katika ngazi mbalimbali za maamuzi.
Walieleza kuwa mafunzo hayo yamewasisitiza kutumia vigezo muhimu wakati wa kufanya uchambuzi wa kiuchumi na
kifedha ili kufikia uamuzi wa kutambua miradi ipi ina manufaa na inaweza kupata
mikopo katika soko la mitaji.
“vigezo
kama mzunguko wa mradi (project cycle) ikiwa ni pamoja na andiko la awali
(concept note), mchanganuo wa faida na hasara (cost-benefit analysis) vigezo
vya kuchanganua mradi kama vile uwezo wa uzalishaji (internal rate of return) na thamani halisi ya uwekezaji (Net Present
Value) vimetolewa ufafanuzi mzuri na vimeeleweka na tumevielewa” Alisema mmoja
wa wakufunzi aliyejulikana kwa jina la Jemsi.
Tume ya mipango
inaendelea na zoezi lake la kutoa mafunzo kwa walengwa wakuu ambao
ni wataalam wa Sera na Mipango ambapo kuanzia Septemba 19 wataalamu wa
mafunzo hayo watakuwa Mkoani mbeya kwa ajili ya zoezi hilo






0 Comments