Random Posts

LUGALO GOLF CLUB BINGWA MASHINDANO YA MKUU WA MAJESHI CDF TROPHY

 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda (kushoto )akimkabidhi zawadi ya Kikombe Mshindi wa Jumla wa Kombe la Mkuu wa majeshi CDF TROPHY mpiga Golf ambaye ni Mkuu wa majeshi Mstaafu Jenerali George Watara mara baada ya mashindano katika Uwanja wa Golf Lugalo Jijini Dar es Salaam jana Septemba 24 .

(Picha na Luteni Selemani Semunyu) .

 Mshindi wa Jumla wa mashindano ya CDF Trophy 2016 Mkuu wa majeshi mstaafu George Waitara (wa kwanza kulia)akipokea Mfano wa Tiketi ya Ndege aliyopewa baada ya kushinda Wapili kulia ni Mnadhimu mkuu wa jeshi Luteni  Jenerali  Venance Mabeyo,watatu Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul  Makonda  na Wakwanza kushoto ni mwenyekiti wa Lugalo Golf Club Brig  Gen Michael Luwongo.

 Mshindi wa Jumla wa mashindano ya CDF Trophy 2016 Mkuu wa majeshi Mstaafu George Waitara (wa kwanza kulia)akipiga mpira wakati wa mashindano  hayo katika uwanja wa Golf Lugalo Dar es Salaam wakwanza kushoto ni katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi Mh Job Masima
 Watoto Junior walioshiriki mashindano ya Kombe la mkuu wa majeshi CDF Trophy wakiwa katika harakati za mchezo huo katika mashindano yaliyofanyika uwanja wa Golf Lugalo jana Jumamosi Septemba 24  Jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya Watoto (Junior) wasichana walioshiriki mashindano ya Kombe la mkuu wa majeshi CDF Trophy wakiwa katika harakati za mchezo huo katika mashindano yaliyofanyika uwanja wa Golf Lugalo jana Jumamosi Septemba 24  Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Watoto( Junior) walioshiriki mashindano ya Kombe la mkuu wa majeshi CDF Trophy wakiwa katika harakati za mchezo huo katika mashindano yaliyofanyika uwanja wa Golf Lugalo jana Jumamosi Septemba 24  Jijini Dar es Salaam.  
Baadhi ya Wachezaji Wanawake( Ladies) walioshiriki mashindano ya Kombe la mkuu wa majeshi CDF Trophy wakiwa katika harakati za mchezo huo katika mashindano yaliyofanyika uwanja wa Golf Lugalo jana Jumamosi Septemba 24  Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Luteni Selemani Semunyu).
.........................................................................................
Na Luteni Selemani Semunyu ,JWTZ
Mpiga Golf na Mkuu wa majeshi Mstaafu George Waitara ameibuka mshindi wa jumla wa mashindano ya CDF Trophy yaliyomalizika Jumamosi  Septemba 24 katika uwanja wa Golf Lugalo Jijini Dar es Salaam baada ya kuwashinda wapiga Golf Zaidi ya 100 walioshiriki mashindano hayo.

Mkuu huyo wa majeshi Mstaafu anayetokea Klabu ya  Lugalo aliibuka mshindi  baada ya kupata Net ya 70 baada ya kupata mikwaju ya Jumla 88 huku kiwango cha uchezaji kikiwa ni 18 na hivyo mbali na kikombe alikabidhiwa Tiketi ya kwenda na kurudi  Abu dhabi.
Akikabidhi zawadi hiyo mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Mh Paul Makonda aliyekuwa Mgeni Rasmi aliahidi kuhakikisha ushirikiano na jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania JWTZ unaendelezwa hasa katika kuendeleza michezo mbalimbali ikiwemo Golf.

Pia aliomba JWTZ katika hatua za kuhamia Dodoma na ujenzi wa Uwanja mpya wa Golf usibadili matumizi ya uwanja wa Awali wa Golf Lugalo ili kutoa nafasi ya kuendeleza mchezo huo lakini kuonyesha historia ya mchezo huo nchini kwa maana ya uwanja ulikoanzia.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo Brigedia jenerali Michael Luwongo alisema wameshafanikiwa kupata hekta 250 Kilometa nane toka Dododoma mjini na Kilometa Mbili toka Barabarani sehemu ambayo wanatarajia kujenga uwanja wa kisasa Zaidi ya wa Awali wa Lugalo.

“Tumepata sehemu hivyo katika kutekeleza Agizo la kuhamia Dododoma tunaenda nalo sambamba na tutajenga uwanja wa Kisasa pia mwaka huu tunafikisha miaka 10 ya Klabu pia tutaandaa mashindano mazuri kuenzi waasisi wa Klabu hiyo” Alisema Brigedia Jenerali Luwongo .

Katika hafla ya Utoaji wa Zawadi na Ufungaji wa Mashindano hayo Mkuu wa Wa majeshi ya Ulinzi  Jenerali Davis Mwamunyange aliwakilishwa na Mnadhimu mkuu wa jeshi Luteni Jenerali Venance Mabeyo .

Katika Makundi mengine Daraja a mshindi S Brown aliyepata Net ya 70,akifuatiwa na Dk Mndolwa aliyepata net ya 73, Daraja B kanali kalino Kondwani aliibuka na ushindi kwa net 70 akifuatiwa na Telens Mwakalukwa aliepata net 72.

Kwa upande wa  Daraja C Alfred Kinswaga  aliibuka na ushindi kwa net 70 akifuatiwa na Kapten Amanji Mandengule kwa Net ya 77 huku Senior akishinda Charles Sanga kwa Net ya 75 akifuatiwa na Salvatory Rwabizi kwa net ya 76.
Wanawake akishinda Clelensia Kavula kwa net 70 wakati wachezaji wasaidizi mshindi ni Richard Tweve kwa net ya 69 akifuatiwa na Reuben Shaban kwa Net ya 70 huku mwanamke pekee kwa kundi hilo Rehema Nyenza akishinda kwa Net ya 87.

Post a Comment

0 Comments