Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akitoa hotuba ya
ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani alioizindua
Kitaifa mjini Geita leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki
Ajali, Tunataka Kuishi”. Katika hotuba yake, Masauni aliwaagiza Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na
aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili
kupunguza ajali za kizembe.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia),
akimsikiliza Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka Makao Makuu, Koplo
Faustina Ndunguru wakati alipokuwa anatoa maelezo jinsi magari mbalimbali yanavyovunja
sheria za barabarani. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa maonyesho hayo
yanayofanyika Kitaifa mjini Geita, Mhandisi Masauni aliwaagiza Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu
na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili
kupunguza ajali za kizembe.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiyaangalia
maandamano ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo yanafanyika Kitaifa katika
Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita, yalipokuwa yanaingia katika viwanja
hivyo kwa ajili ya kuadhimisha wiki hiyo. Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara
nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na
aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili
kupunguza ajali za kizembe.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimpa
zawadi ya Kombe la Ushindi wa kwanza Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge jijini
Dar es Salaam, Veronica Innocent, ambaye alishinda nafasi ya kwanza katika
uchorani wa picha zinazoonyesha usalama barabarani ambayo zilipambanishwa
katika shule za Mkoa wa Dar es Salaam na Geita. Masauni aliyazindua Maadhimisho
ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, ambayo yanafanyika Kitaifa, katika
Viwanja vya CCM Kalangalala, mjini Geita. Masauni katika hotuba yake aliwaagiza
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika
Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama
barabarani ili kupunguza ajali za kizembe.
Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, ambaye pia ni Katibu wa Baraza la
Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga akizungumza katika
maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inayofanyika Kitaifa katika
Viwabya vya CCM Kalangalala mjini Geita. Maadhimisho hayo yalizinduliwa na
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la
Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia).
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.





0 Comments