MLIMBWENDE Laura
Kwai kutoka Chuo Kikuu cha Iringa amefanikia kunyakua taji la TTCL Miss
Higher Learning 2016 akiwabwaga washiriki wenzake Evelyn Andrew
aliyeshika nafasi ya pili na Clara Nyaki aliyekuwa watatu.
Mashindano
hayo yaliyofanyika Jana usiku katika Ukumbi wa King Solomon yaliweza
kufana hasa baada ya kuwa na ushindani wa hali ya juu baina ya warembo
hao.
Katika meza ya Majaji
iliyoongozwa na Hasheem Lundenga iliweza kufanya kazi kubwa kwa kuweza
kuwataja washiriki walioingia tano bora na hatimaye mshindi wa TTCL Miss
Higher Learning 2016 kuwataja Washiriki waliofanikiwa kuingia ni tano
bora ambao Mariam, Lucy Ludy, Evelyn Andrew, Laura Kwai na Clara Nyaki .
Mshindi
wa kwanza amejinyakulia kiasi cha shilingi Milioni Moja taslimu
(1,000,000) pamoja Scholarship ya kusoma katika Chuo chochote, mshindi
wa pili amejinyakulia milioni moja taslimu (1,000,000)na mshindi wa tatu
amepata Laki saba (700,000) taslimu na kwa Washiriki waliobaki kila
mmoja atakabidhiwa kiasi cha laki mbili kila mmoja (200,000).
Tanzanite
International Film Festival (TAIFF) walimtaja Laura Kwai na Rhoda Iddy
Kama mabalozi wao katika kuyatangaza madini ya Tanzanite ndani na nje
huku TTCL wakimtaja Glory Gideon kama balozi wao kwa muda wa mwaka
mmoja.
Walimbwende walioshiriki
kinyang'anyiro cha Kumsaka TTCL Miss Higher Learning 2016 ni Glory
Gideon (Chuo cha Usimamizi wa fedha IFM), Lucy Ludy (Taasisi ya Ustawi
wa Jamii), Jonatha Joram (Chuo cha Usimamizi wa fedha IFM), Clara Nyaki
(Taasisi ya Ustawi wa Jamii), Rhoda Iddy (CBE), Evelyne Andrew (Taasisi
ya Ustawi wa Jamii), Tamita Mwakitalu (Chuo cha Utumishi wa Umma,
Magogoni), Jackline Everist (Chuo cha Usimamizi wa fedha IFM), Nasra
Muna (Chuo cha Usimamizi wa fedha IFM) Laura Kwai (Iringa University),
Mariam J Mwita (Chuo cha utumishi wa Umma, Magogoni), Emmaculate Kasinsa
(Chuo cha utumishi wa Umma, Magogoni), Victoria Shiyo (CBE), Farida
mlawa (UDOM), Lilian Kaishozi (UDOM).




0 Comments