Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea msaada wa
fedha kiasi cha dola laki mbili (USD
200,000) kutoka kwa Balozi wa Uganda hapa nchini Doroth Samali Hyuha wapili
kutoka (kushoto) akiwa pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda
Elibariki Maleko. Msaada huo umetolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni
kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa Tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi mchango wa fedha
kiasi cha dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) uliotolewa na Rais wa
Uganda Yoweri Kaguta Museveni Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kusoma taarifa kuhusu Tetemeko la ardhi
lililotokea mkoani Kagera.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akifatilia kwa makini taarifa iliyokuwa ikitolewa na Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa kuhusu Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara
baada ya kupokea taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera kutoka
kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akisoma taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani
Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Uganda
hapa nchini Doroth Samali Hyuha mara baada ya kuwasilisha mchango wa kiasi cha
fedha Dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) kutoka kwa Rais wa Uganda
Yoweri Museveni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akimshukuru Naibu Balozi wa Kenya hapa nchini Boniface
Muhia mara baada ya kupokea salamu za pole kutoka kwa Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta na kwa misaada mbalimbali ambayo inatarajiwa kuwasili mkoani Kagera kutoka
Kenya muda wowote.
PICHA ZOTE NA IKULU








0 Comments