Mwenyekiti wa Bunge Sports Club Mhe. William Ngeleja akizungumza na waandishi
wa Habari(hawapo pichani) kuhusu mechi ya kesho kati ya wabunge mashabiki wa
Simba na Yanga na Wasanii wa Bongo Flava na Bongo Movies katika Uwanja wa Taifa na kutangaza kuwa mgeni rasmi
katika mechi hiyo atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa.
Mwenyekiti wa Bunge Sports Club Mhe. William
Ngeleja akionesha moja ya kikombe kwa waandishi wa Habari(hawapo pichani) kitakachotolewa
kwa mshindi katika mechi ya kesho kati ya wabunge mashabiki wa Simba na Yanga
na Wasanii wa Bongo Flava na Bongo Movies katika Uwanja wa Taifa.
Mwakilishi wa wasanii wa Bongo Movie Bw.William
Mtitu akizungumza kuhusu maandalizi ya timu yao kabla ya mchezo wao wa kesho na
wasanii wa Bongo Flava utakaofanyika katika Uwanja wa Taifa kwa dhumuni la
kuchangisha fedha kwaajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Mwakilishi kutoka Mwananchi Communications
LTD Bw. Francis Nanai akizungumzia mchango wao walioutoa wa kutoa taarifa kwa
watanzania kuhusu hali ilivyo mkoani Kagera na kutoa nafasi kwa makampuni
yatakayojotokeza kufanya harambee kuwasaidia waathirika wa tetemeko watatoa
matangazo bure kwa ajili yao katika vyombo vyao vya habari.
Mwakilishi kutoka Shirika la Bima ya Afya
Taifa Bw. Baraka Maduu akitoa ufafanuzi kuhusu huduma za kiafya zitazotolewa
kwa wachezaji na wananchi kwa ujumla kesho katika mchezo kati ya wabunge
mashabiki wa Simba na Yanga Wasanii wa Bongo Flava na Bongo Movies.
Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Bunge
Mhe. William Ngeleja akipokea hundi ya shilling million kumi kutoka kwa Mwakilishi
wa Mwananchi Communications LTD Bw. Francis Nanai kwa ajili ya msaada kwa msadaa
kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Bunge
Mhe. William Ngeleja akipokea hundi ya shilling millioni tano kutoka kwa Mwakilishi wa Jubilee Insurance Bi. Elieth
kileo kwa ajili ya msaada kwa msadaa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani
Kagera.
Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Bunge
Mhe. William Ngeleja akipokea hundi ya shilling millioni tano kutoka kwa Mwakilishi wa Jubilee Insurance Bi. Elieth
kileo kwa ajili ya msaada kwa msadaa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani
Kagera.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia
mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Bunge
Mhe. William Ngeleja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo
kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge wakiwa katika
picha ya pamoja na wabunge, wasanii wa bongo movie na bongo flava, wawakilishi
wa Mwananchi Communications Ltd, Jubilee Insurance,Shirika la Taifa la Bima ya
Afya na Selcom Tanzania mara baada ya mkutano wa kuhamasisha wananchi kushiriki
kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera kupitia michezo.
(Picha Zote na Raymond Mushumbusi WHUSM.)










0 Comments