Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga.akizungumza.
.........................................................................................................
NA VICTOR MASANGU
MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo Mohamed Mwanga amesema kuwa
atahakikisha anazisimamia na kuzivalia
njunga ipasavyo fedha amabzo zinazotolewa
na halmashauri kwa ajili ya kuweza kuwasadia vijana na wakinamama lengo ikiwa
ni kuona zinatumika katika vikundi mbali lli kuweza kukuza uchumi na kuleta chachu ya
kimaendeleo.
Mwanga ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akihojiwa na
kituo kimoja cha redio cha Jijini Dar es Salaam kuhusina na changamoto mbali mbali zilizopo katika utendaji wa kazi
pamoja na mikakati kabambe aliyoiweka
katika kuwahudumia wananchi wake wa Bagamoyo.
Alisema kwamba halmashauri zinanapaswa kutenga kiasi cha
asilimia kumi cha makusanyo ya mapato yake ambapo vijana wanatakiwa kupatiwa
asilimia tano na kwa upande wa wakinaamama wanatakiwa wapatiwe asilimia tano
kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao za ujasiriamali.
“Mimi kama mkuuwa Wilaya ya Bagamoyo mikakati yangi ni
kuhakikisha kwamba fedha hizo ambazo ni asilimia kumi zinawafikia walengwa wote
bila ya kuwa na ubaguzi, hivyuo nitazisimamia na kuona ni jinsi gani zinaweza
kuleta mabadiliko chanya kwa vijana pamoja na wakinamama ambao watapatiwa fedha
hizo,”alisema Mwanga.
Aidha mkuu huyo alisema kwamba ana imani kwamba eendapo
halmashauri ikilitilia mkazo suala hilo la kuhakikisha kiais hicho cha asilimia
kumi kinatolewa katika kila bajeti kutaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa
kuviwezesha vikundi vya aina mbali mbali ili viweze kuendesha biashara zao na
kukuza mitaji waliyonayo.
Pia alifafanua kuwa fedha hizo zinatolewa kwa uataratibu
maalumu ambapo inatakiwa vijana au wakinamama kuunda vikundi vyao na kuvisajili
ili pindi fedha hizo zinapotolewa ziweze kuwafikia walengwa kwa wakati na
kuweza kuwanufaisha kwa kiais kikubwa katika
kuendeleza biashara zao ambazo wanakuwa wanazifanya ziweze kukua zaidi.
“Katika Wilaya yangu
ya Bagamoyo kwa sasa nina halmashauri mbili, ambapo kuna halshauri ya bagamoyo,
pamoja na halmashauri ya mji mdogo chalinze, kwa hivyo zote hizi zinatakiwa
kutenga asilimi hiyo kumi kwa ajili ya kuviwezesha vikundi hivyo nbila ya kuwa
na upendeleo wa aiana yoyote,”aliongeza Mwanga.
Alisema kwamba kwa sasa kuna fedha ambazo tayari
zimeshatolewa na halmashauri kwa ajii ya
kuvisaidia vikundi hivyo vya wakinamama na vijana, ambapo katika halmashauri ya
bagamoyo kumeshatolewa kiasi cha shilingi milioni 120 na kuongeza kuwa fedha
hizo zitakuwa zinatolewa kwa mzunguko ii ziweze kuwafikia walengwe wote.
Katika hatua nyingine Mwanga alitoa wito kwa vijana na
wakinamama ambao watapata fursa ya kupatiwa fedha hizo kuhakikisha kuwa wanazitumia vizuri katika kuendeshea biashara
zao ili kuweza kukuza mitaji yao na kuondokana na kuwa tegemezi.

0 Comments