Mcheza golf Mtoto Asnath Juma akiwa katika harakati za
kupiga mpira katika mashindano yaliyohusisha vijana katika uwanja wa Klabu ya
jeshi la Ulinzi la Wananchi ya Lugalo jijini Dar es Salaam .
(Picha na Luteni
Selemani Semunyu).
Wacheza golf Watoto wa Klabu ya Lugalo wakiwa katika
picha ya pamoja katika mashindano
yaliyohusisha vijana wadogo katika uwanja wa Klabu ya jeshi la Ulinzi la
Wananchi ya Lugalo jijini Dar es Salaam.
......................................................................................................................
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
Mashindano ya mwisho wa Mwezi ya Mchezo wa Golf katika Klabu jeshi la ulinzi la
Wananchi wa Tanzani a ya Lugalo
yamefanyika huku Wachezaji wengi wakichezea viwango vipya vya Uchezaji baada ya kufanya vizuri au
vibaya katika mashindano ya Arusha Open na yale ya PWC yaliyofanyika Lugalo
Jijini Dar Es Salaam.
Katika Division A mshindi ni Juma L ikuli aliyep0iga mikwaju
ya jumla 76 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 5 akifuatiwa na Saleh Mcharo
kwa count back baada ys kupiga mikwaju ya jumla 77 huku
kiwango cha uchezaji kikiwa ni Sita.
Katika Division B Raji Lavingia aliyeshinda baada ya
kufungana (count back) baada ya kupiga mikwaju ya jumla 69 huku kiwango chake
cha Uchezaji kikiwa ni 14 akifuatiwa na Shaizad Bhanji aliyepiga mikwaju ya
jumla 69 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 18.
Katika Kundi Cmcheza Golf Enock Magile aliibuka na Ushindi baada kupiga mikwaju ya
Jumla 72 akifuatia na Faidhal Mawji ambaye alishindaa baada ya kufungana (Count
back ) baada ya kupiga Mikwaju ya Jumla 77 huku kiwango chake cha uchezaji
kikiwa ni 24.
Kundi la wazee Senior
katibu Mkuu wa Wizara ya ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima
aliibuka na ushindi baada ya kupiga
mikwaju ya jumla 70 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 18 Akifuatiwa na
Dk Edmund Mndolwa aliyepiga mikwaju ya jumla 78 huku kiwango chake cha uchezaji
kikiwa ni Saba.
Kwa Upande wa Wanawake mshindi ni Sophia Mathias aliyepiga
mikwaju ya Jumla 74 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 11 akifuatiwa na
Vicky Elias aliyepiga mikwaju ya jumla 78 huku kiwango chake cha uchezaji
kikiwa ni Nane.
Na kwa Upande wa Watoto George Kapinga aliibuka Mshindi
baada ya kupiga Mikwaju ya Jumla 71 huku kiwango chake cha uchezaji kikiwa ni 16
akifuatiwa na Mpiga Golf Zabron Khamis aliyepiga mikwaju ya Jumla 72 huku
kiwango chake cha Uchezaji kikiwa ni 20.


0 Comments