Bondia wa ngumi za kulipwa nchini
Tanzania, Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ amemkalisha Mchina Chengbo Zheng kwa
raundi ya kwanza tu ,pambano hilo la raundi 10 limefanyika kwenye Ukumbi wa
Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na lilikuwa linasubiriwa kwa hamu kwa kuwa
kila bondia alijitapa awali kuwa atamkalisha mapema mwenzake.
Wakati watu walikosa burudani ya
pambano la utangulizi la Cosmas Cheka dhidi ya Jason Bedemen raia wa Afrika
Kusini ambaye aligoma akidai amebadilishiwa bondia na pambano lake kuondolewa
ubingwa, hivyo nguvu zote zikaelekezwa kwenye pambano la Dulla Mbabe na Mchina
huyo.
Wakati wengi waliamini pambano
litakuwa na ushindani mkali, Dulla alishambulia kwa kasi na kumuangusha Zheng
ambaye alijikongoja na kuendelea.
Lakini ikionekana kama atatulia,
Dulla alimsogeza kona na kupeleka ngumi nne mfululizo ambazo zilimbaliza na
kumaliza pambano kwani baada ya Zheng kwenda chini, hakuweza kuinuka tena na
ikawa kwaheri.

0 Comments