...............................................................................................................
Na.Alex Mathias.
Timu
ya Simba hatimaye imevunja mwiko katika uwanja wa CCM Kambarage kwa
kupata ushindi wa kwanza mbele ya Mwadui FC kwani tangu wachimba madini
hao walikuwa hajapoteza mbele ya Mnyama mchezo wa Ligi kuu ya Tanzania
kwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-0.
Kabla ya mchezo wa leo, Simba na ilishindwa kupata ushindi katika
mechi mbili za msimu uliopita huku ikichezea kichapo cha goli 1-0 kwenye
uwanja wa taifa wakati wa mchezo wa marudiano. Mchezo wa kwanza
uliozikutanisha klabu hizo ulipigwa kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga
na Simba kulazimishwa sare ya kufungana goli 1-1.
Ibrahim Mohamed amefanikiwa kufunga kwa mara ya kwanza tangu
aliposajiliwa kujiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar. Ibrahim amefunga
magoli mawili na kusaidia goli moja lililofungwa na Shiza Kichuya.
Hadi sasa, wachezaji wote waliosajiliwa na Simba msimu huu wakitokea
Mtibwa Sugar ,Mzamiru Yassin [4], Ibrahim Mohamed[2] na Shiza Kichuya
[8] wote wameshaifungia Simba jumla ya mabao 14 kwa ujumla wao.
Kichuya bado ameendelea kupasia kamba katika mfululizo wa mechi za
ligi kuu Tanzania bara, tayari ameshapasia nyavuni mabao 8 magoli
mawili mbele ya Amis Tambwe wa Yanga mwenye magoli 6 katika orodha ya
wafungaji wa VPL hadi sasa. Kichuya pia anaongoza kwa kutupia nyavuni
ndani ya klabu yake.
Simba inaendelea kuongoza ligi ikiwa na pointi 32 baada ya kucheza
mechi 12 hadi sasa huku ikiendeleza rekodi yake ya kutopoteza mchezo,
imeshinda mechi 10 na kutoka sare mara mbili.
Ligi hiyo inatarajia
kuchezwa kesho Jumapili kwa michezo miwili kuchezwa uwanja wa Mabatini
na Uhuru jijini Dar es salaam Yanga wakiwa na Kocha wao Mkuu Hans Van
Der Pluijm watawaalika wakata mbao Timu ya Mbao FC toka Mwanza.

0 Comments