Naibu
Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na serikali za mitaa, Selemani
Jafo akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Kilamba,
kushoto ni Mbunge wa Mbagala, Issa Mangungu.
Mkuu
wa wilaya ya Temeke na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke wakimsikiliza
kwa makini Naibu Waziri alipotembelea shule ya Kilamba kuangalia
utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa.
.......................................................................................
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani
Jafo amewapongeza viongozi na watendaji wa wilaya ya Temeke kwa kutekeleza
maagizo yake aliyoyatoa mwezi mmoja aliopita ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanafunzi
wanakaa kwenye madawati na kuongezwa vyumba vya madarasa.
Mnamo
mwezi Septemba mwaka huu, Jafo alizitembelea shule nne za wilaya ya Temeke
zilizopo eneo la mbagala na kukutana na changamoto lukuki, zikiwemo
kutotembelewa shule hizo na Afisa elimu wilaya toka mwaka huu uanze kitendo
kilicho sababisha kutobainika kwa changamoto ili zipatiwe ufumbuzi.
Shule
alizozitembelea ni pamoja na shule za msingi Chemchem, Nzasa, Charambe, na Kilamba
ambapo Jafo alikuwakuta watoto wa darasa la saba pekee kwa shule ya Chemchem
ndio waliokuwa wakikalia madawati.
Katika
shule ya nzasa, Naibu Waziri huyo aliwakuta watoto wamejazana huku kukiwa hakuna
mpango wowote wa ujenzi wa madarasa.
Aidha aliwakuta walimu wakiwa hawana ofisi ya
walimu licha ya shule hizo kuwa katika jiji la biashara lenye mapato mengi.
Hata
hivyo, Shule ya Kilamba pekee ndiyo ilikuwa katika hali ya kuridhisha, na baada
ya ziara hiyo alitoa maagizo kwa mkurugenzi wa Temeke kuzifanyia kazi
changamoto alizo zibaini kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Jafo alifanya tena ziara kwenye eneo hilo ili
kubaini utekelezaji wa maagizo yake na katika safari hiyo ya pili alifanikiwa
kuzitembelea shule alizozitembelea awali pamoja na shule mbili nyingine za
Kiburugwa na Kinguki.
Alipofika
alikuta watoto wote wakiwa katika madawati pamoja na kuanza kwa harakati za
kuongeza madarasa na ujenzi wa ofisi za walimu kwa shule hizo ambazo baadhi
zilikuwa hazina.
Kadhalika,
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, alimpa taarifa Jafo kuwa shule ya nzasa
itapata jumla ya vyumba saba, Chemchem vyumba vitano, chalambe vyumba
vinne na ofisi ya walimu na kilamba kujengewa fensi ya shule.
Naibu
Waziri huyo aliwashukuru na kuwapongeza viongozi wote wa temeke kwa kujali
matatizo ya jamii.
Katika
ziara hiyo Jafo aliongozana na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Mbunge wa jimbo la
Mbagala Issa Mangungu, Meya ya Temeke Chaurembo, Mkurungenzi wa Manispaa ya temeke
na wakuu wake wa idara huku akisema viongozi hao ni mfano wa kuigwa.


0 Comments