Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara
ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Joyce Hagu akifafanua jambo wakati wa
ufunguzi wa semina ya wasanii wa muziki wa singeli jana Jijini Dar es
Salaam,kulia ni Meneja Mkuu wa EFM Bw.Denis Ssebo na kushoto ni Mkurugenzi wa
EFM Bw. Francis Ciza.
Mkuu wa Matukio ya Sanaa wa Baraza la Sanaa la
Taifa(BASATA),Bw.Kuwijira Maregesi akiongea na waasanii kuhusu maadili ya
utunzi wa mashairi wa nyimbo zao wakati wa ufunguzi wa semina ya wasanii wa
muziki wa singeli iliyoandaliwa na uongozi wa Radio ya EFM jana Jijini Dar es
Salaam kushoto ni Afisa Sanaa Bi. Bona Masenge na kulia ni Mkurugenzi wa Radio
EFM Bw.Francis Ciza.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA),Bw.Innocent Mungi akiwasisitiza wasanii (hawapo katika picha)
matumizi sahii ya mitandao ya kijamii wakati wa semina ya wanamuziki wa singeli
iliyoandaliwa na uongozi wa Radio ya EFM jana Jijini Dar es Salaam.
Meneja Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Bibi.Valentina Baltaz akiongea kuhusu umuhimu wa wasanii
kulipa kodi kupitia kazi zao za sanaa ili kuchangia pato la taifa wakati wa
semina la wasanii wa muziki wa singeli iliyoandaliwa na uongozi wa Radio ya EFM
jana Jijini Dar es Salaam kulia ni Mhariri
Mkuu wa EFM Bi.Scholastica Mazula.
Afisa Sanaa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA) Bi.Bona Masenge akiongea na wasanii(Hawapo katika Picha) kwa kuwataka
kutunza na kuendeleza utamaduni wa kitanzania kwa kufuata taratibu na sheria
katika kazi zao za sanaa wakati wa semina ya wasanii wa muziki wa singeli leo
Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Taasisi ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA),Bw.Innocent Mungi na kulia ni Mkuu wa Matukio ya Sanaa wa
Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA),Bw.Kurwijira Maregesi
Baadhi ya Wasanii wa Muziki wa Singeli
waliohudhuria semina iliyoandaliwa na uongozi wa radio EFM kwa lengo la
kuwapata somo la kuifanya sanaa kuwa ujasiliamali ikiwemo kupata mbinu
mbalimbali za uwekezaji .
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari Utamaduni,Sanaa na
Michezo Bi.Joyce Hagu(wa tano kutoka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya
pamoja na wasanii wa muziki wa singeli baada ya semina iliyokuwa imeandaliwa na
uongozi wa Radio EFM jana Jijini Dar es Salaam.
Picha
na Lorietha Laurence
................................................................................
Na
Lorietha Laurence-WHUSM
Wasanii
wa Muziki wa Singeli wameaswa kuzingatia mafunzo ya sanaa ya ujasiliamali
yatakayowasaidia kuongeza weledi na mbinu
za kukuza kazi zao na hatimaye kuwa na sanaa bora kwa ukanda wa Afrika Mashariki.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya
Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Joyce Hagu wakati wa ufunguzi wa semina ya
wasanii wa muziki wa singeli jana Jijini Dar es Salaam.
Bi
Joyce aliongeza kwa kusema kuwa sanaa ya muziki ni kazi kama kazi nyingine
hivyo ni budi kusimamia misingi iliyo bora inayoendana na utamaduni wa
kitanzania katika utunzi wa tungo za singeli.
“Utamaduni
ni mali ya jamii hivyo ni jukumu letu sote kupenda,kuthamini na kuendeleza
utamaduni wetu kupitia kazi za sanaa na hii itasaidia kutekeleza kwa vitendo
Sera ya Taifa ya Utamaduni” alisema Bi.Joyce.
Aidha
aliupongeza uongozi wa EFM kwa kuandaa semina hiyo ambayo imewapa fursa wasanii kupata elimu
ya msingi kuhusu muziki na kuifanya kazi ya sanaa kuwa ya thamani kwa jamii.
Naye
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA),Bw.Innocent Mungi amewataka wasanii hao kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa kuuza kazi zao
za mziki na hivyo kuwa na soko la kimataifa na sio kutumia mitandao kwa ajili
ya kuchafuana.
Kwa
Upande wake Mkuu wa Matukio ya Sanaa wa Baraza la Sanaa la
Taifa(BASATA),Bw.Kuwijira Maregesi amewakumbusha wasanii hao umuhimu wa kuzingatia maadili pale wanapofanya
utunzi wa nyimbo zao ili kuepuka usumbufu wa kufungiwa.
Mbali
na mada ya maadili wasanii walipata fursa ya elimu ya mlipa kodi kutoka kwa Meneja Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Bibi.Valentina Baltaz ambapo aliwaeleza wasanii umuhimu
wa kulipa kodi kupitia kazi zao za sanaa kulingana na sheria na taratibu za
nchi ili kuchangia katika kukuza pato la
taifa.
0 Comments