.....................................................................................................
Na.Alex Mathias.
Uongozi
wa timu ya soka ya Kagera Sugar umesema kwamba bado una inami na kocha
mkuu wa klabu hiyo Mecky Mexme licha ya baadhi ya mashabiki kuonyesha
mabango ya kutokuwa na imani nae ya kuendelea kusalia ndani ya kikosi
cha timu hiyo.
Mwenyekiti
wa Kagera Sugar Salum Madaki, amesema kuwa kwanza anashangazwa na
mashabiki wa timu hiyo kudiriki kubeba mabango ambayo hayana msingi
kwani kwa hali ilivyo kocha wao anastahili kupewa sifa kwa jitihada
kubwa alizozifanya za kuhakikisha timu bado ipo katika nafasi za juu
kwenye msimamo wa ligi tofauti na msimu uliopita.
Madaki
amesema kuwa mashabiki wa timu hiyo wasigetemee kuondoka kwa Mexme
ndani ya kikosi hicho kwa wakati huu kwani uongozi bado unaridhishwa na
ufundishaji wake licha ya kupoteza michezo miwili mfululizo ikiwemo
dhidi ya Azam ambapo walikubali kufungwa kwa jumla ya mabao 3-2 huku
wakiwa wametoka kufungwa na Yanga mabao 6-2.
Na Mpaka sasa Kagera
Sugar ipo nafasi ya tano wakiwa na alama 18 na tofauti na Msimu
uliopita kwani ilijinasuwa kushuka daraja hivyo mashabiki watulie kwani
Mexime ni kocha bora hapa nchini Tanzania.

0 Comments