Timu
ya KRC Genk imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Westerlo mchezo wa
Ligi Kuu ya Ubelgiji inayojulikana 'Jupiler League mechi hii imechezwa
kwenye uwanja wa Laminus Arena.
Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa
hazijafunga kutokana na uimara wa ulinzi pamoja na washambuliaji
kutokuwa makini wanapopata nafasi ya kufunga.
Dakika ya 54 Genk
walipata bao la kwanza kupitia kwa Alejandro Pozuelo akipokea pasi safi
kupitia Leon Bailey na 66 mshambuliaji anayemuweka benchi Samatta Nikos
Karelis alifunga la pili naye akipokea mpira toka kwa Mjamaica Leon
Bailey aliye kwenye fomu ya hali ya juu.
Baada
ya kufunga bao Karelis alitolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na
Mbwana Ally Samatta na katika dakika ya 82,Jamo Molenberghs aliifungia
Westerlo bao la kufutia machozi hadi kipyenga kina pulizwa Genk
wameibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Aidha huo
unakuwa mchezo wa 31 kwa Samatta tangu amejiunga na Genk Januari mwaka
huu kutoka TP Mazembe ya DRC, 18 msimu uliopita na 12 msimu huu,
akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita.
Katika
mechi hizo, ni 16 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na tano msimu
huu, wakati 14 alitokea benchi nane msimu uliopita na 11 msimu huu na
mechi tisa hakumaliza akitolewa, sita msimu uliopita na tatu msimu huu.
Kwa
matokeo hayo KRC Genk wamepanda hadi nafasi ya 6 katika msimamo wa
Jupiler League wakiwa na alama 20 huku wakiwa wameruhusu kufungwa mabao
18 na wao wakiwa wamefunga mabao 17 na wakiwa wamecheza jumla ya mechi
13,sare miwili,kufungwa michezo mitano na kushinda sita.

0 Comments