| Sharik Chughule |
Na Mwandishi Wetu
......................................
Mwenyekiti
wa CCM, Shina la Pamba Road, Dar es Saaam, Sharik Choughule, amewaasa
vijana kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa kufanya kazi za
kujiajiri.
Amesema,
kufanya hivyo kutawawezesha vjana wengi kuwa na ajira za uhakika,
badala ya kusubiri ajira za serikali au taasisi mbalimbali kwa kuwa
nafasi za ajira katika sekta hizo ni chache huku mahitaji yakiwa ni
makubwa.
Choughule
ambaye pia ni Kamanda wa Vijana Kata ya Kivukoni, Dar es Salaam,
amesema hayo leo wakati akizungumzia kumbukumbu ya miaka 17 ya Kifo cha
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambayo Maadhimisho yake
yanafayika leo Kitaifa mkoani Simiyu kwa shughuli ya kuzima Mwenge.
Amesema,
ili kuweza kufanya kazi za kujiajiri, vijana ni lazima kwanza kuondoa
woga, ili kujiamini kuwa wanaweza kwa kuwa ajira binafsi zipo nyingi
hasa ikizingatiwa kwamba wengi siku hizi wana elimu za kutosha hadi za
viwango vya Chuo Kikuu.
"Vijana
lazima tujiamini kwa kuwa sisi ndiyo tegemeo la taifa, hivyo siyo
busara vijana kuanza kulalamika kuwa hatuna ajira kwa lengo la kutarajia
kuwa Taifa ndilo tulitegemee kutupatia ajira, hayo si mawazo mwafaka
kwa afya ya nchi yetu", alisema Shoughule.
Alisema,
hatua ya vijana kuanza kuweka kisingizio cha ukosefu wa ajira za
kuajiriwa, kinawadumaza vijana na kukosa maamuzi ya kubuni au kukosa
ubunifu wa kubuni miradi aina tofauti tofauti kwa manufaa yao.
Choughule
alisema, hivi sasa umefikia wakati wa vijana kuachana na mawazo mgando,
kwa wasababu baadhi ya vijana ambao wameonyesha uthubutu, wameweza
kujiajiri katika sekta za mitandao ya mawasiliano ambayo ni sekta
imeenea duniani kote.
Alisema,
mfano mzuri wa kuigwa ni vijana walipo Jeshi la Kujenga Taifa, JKT,
ambao wamekuwa wakionyesha kufanya kazi nyingi ambazo siyo za kuajiriwa
ikiwemo kuanzisha shughuli za kilimo cha kisasa, ufugaji na ufundi wa
aina mbalimbali ikiwemo kutengeneza samani na ujenzi wa nyumba.
Choghule
amesema, hatua ya vijana kufanyakazi za kujiajiri siyo tu watakuwa
wamemuenzi Baba wa taaifa Mwalimu Nyerere, lakini pia watakuwa
wamemuunga mkono Rais Dk John Magufuli katika azma yake ya kukuza uchumi
wa taifa kwa kaulimbiu yake ya 'Hapa kazi tu'.
0 Comments