Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu(kushoto)
akisikiliza taarifa kuhusu kituo cha TEMESA Mkoa wa Shinyanga kutoka kwa Meneja
wa TEMESA Shinyanga Mhandisi Riziki Lukali, alipotembelea kituoni hapo katika
ziara yake katika vituo vya TEMESA Kanda ya Ziwa.
Mtendaji Mkuu TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu akikagua chumba cha kuhifadhia
vipuri vya matengenezo ya magari TEMESA Mkoa wa Shinyanga, alipotembelea
kituoni hapo katika ziara yake katika vituo vya TEMESA Kanda ya Ziwa.
Mtendaji
Mkuu TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (wa pili
kulia) akitoa maelekezo kwa watendaji wa kituo cha Shinyanga alipotembelea
kituoni hapo katika ziara yake katika vituo vya TEMESA Kanda ya Ziwa.
Mtendaji
Mkuu TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (menye
shati la rangi ya bluu)akiangalia gari la TANESCO Shinyanga, linaloshikiliwa na
TEMESA Shinyanga kwa sababu ya deni la Sh Millioni 96 kushoto ni Meneja wa
TEMESA Shinyanga Mhandisi Riziki Lukali.
Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Shinyanga.
.......................................................................................
Na
Theresia Mwami TEMESA Shinyanga
Wakala
wa Ufundi na Umeme TEMESA Mkoa wa Shinyanga inazidai Halamashauri, Mashirika na
Taasisi za Serikali mkoani humo jumla ya shillingi 163,269,269.82 kutokana na
kupata huduma ya matengenezo ya magari.
Katika
taarifa yake kwa Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Meneja wa TEMESA Shinyanga Mhandisi
Riziki Lukali amesema madeni hayo ni ya mwaka wa fedha 2016/2017 na wamesha
wasilisha madai yao kwa wahusika na wanasubiri kulipwa.
Mhandisi
Riziki Lukali aliwataja wadaiwa hao kuwa ni TANROADS Shinyanga Sh 24,193,733.21,
TANESCO Shinyanga Sh Milioni
96,267,987.63, DED Kishapu Sh 6,753,735.03, RAS Shinyanga Sh 2,742,097.36,
KUWASA Kahama Sh 9,855,714, KASHUWASA Shinyanga Sh 1,992,430, TBA Shinyanga Sh 5,103,062.56,
Mahakama Kuu Shinyanga Sh 5,470,628.91, Uhamiaji Shinyanga Sh 896,333.63, DAS
Kishapu Sh 1,071,573.57, NSSF Shinyanga Sh3,798,184 pamoja na RMO Shinyanga shilingi
5,123, 789.92 milioni na jumla ya madeni hayo yote ni Sh 163,269,269.82.
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu
amefurahishwa na utaratibu wa TEMESA Shinyanga wa kuzuia magari ya taasisi, halmashauri na mashirika yanayodaiwa
na kituo hadi hapo yatakapolipiwa gharama za matengenezo.
Na
pia amemuagiza Meneja wa TEMESA Shinyanga kutoa taarifa kwake kama kuna Taasisi
za Serikali ambazo hukiuka Sheria kwa kutopeleka magari yake kwenye karakana za
TEMESA na kupeleka magari hayo kwenye
karakana binafsi zilizomo mkoani humo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa
dhidi yao.
Dkt
Mgwatu amesisitiza watumishi kuendelea kujituma kufanya kazi kwa weledi na kwa
ubora zaidi ili karakana iweze kuvuta wateja wengi na kuongeza pato la kituo.
Aidha
TEMESA Shinyanga kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 kituo kimepanga kukusanya
jumla ya Sh 458,160,000 kutokana na madeni na huduma zinazoendelea kutolewa
kituoni hapo.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yupo katika ziara ya
kutembelea vituo vya TEMESA vilivyopo Kanda ya Ziwa ili kubaini changamoto
mbali mbali zilizomo na kuzitafutia ufumbuzi.




0 Comments