Kamishna
Jenerali wa Magereza - CGP. John Casmir Minja(vazi la kiraia) akiwa ameongozana
na Mkuu wa Gereza Karanga, Moshi, ACP. Hassan
Mkwiche (kushoto) pamoja na Kaimu Mkuu wa Kiwanda cha Viatu Karanga, ASP.
Michael Minja(kulia) alipotembelea Kiwanda hicho ili kuona eneo lililotengwa
kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda kipya cha
kisasa cha viatu leo Oktoba 14, 2016. Wengine pichani ni Maafisa wa Jeshi
la Magereza Mkoani Kilimanjaro.
Kamishna
Jenerali wa Magereza - CGP. John Casmir Minja(vazi la suti) akiangalia eneo
ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda kipya cha viatu .
Kamishna
Jenerali wa Magereza - CGP. John Casmir Minja(vazi la suti) akipata maelezo
kutoka kwa Mkuu wa Magereza Mkoa Kilimanjaro, ACP. Anderson Kamtearo(kulia)
alipokagua moja ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho
kipya cha kutengeneza viatu.
Eneo
litakalojengwa kiwanda kipya cha kisasa cha kutengeneza bidhaa mbalimbali za
ngozi. Kiwanda hicho kitakuwa cha ubia baina ya Shirika la Magereza na Mfuko wa
jamii wa PPF.
Kamishna
Jenerali wa Magereza - CGP. John Casmir Minja akiangalia kiatu aina ya buti
ndefu zinazotengenezwa kiwandani hapo kwa ajili ya Maafisa na Askari wa Vyombo
vya Ulinzi na Usalama kama inavyoonekana katika picha.
(Picha zote na Lucas Mboje
wa Jeshi la Magereza).





0 Comments