Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Hamad
Masauni, (mwenye tisheti nyekundu) akielekea kutizama mpaka wa Tarekea wilayani Rombo ili kujionea changamoto
zinazotokana na mipaka hiyo pamoja na kutoa maagizo kwa viongozi wanaohusika
kuimarisha ulinzi wa mpaka huo ili kukabiliana na upitishaji wa bidhaa za
magendo pamoja na wahamiaji haramu ambao wamekua wakiinia nchini bila vibali.
Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimaanjaro Kamishna
Msaidizi Mwandamizi Wilbrod Muutafungwa akifatiwa na Kamishna wa Uhamiaji Mkoa
wa Kilimanjaro, Mwanguku, na wan ne kutokea kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Rombo
Agnes Hokororo alieambatana na Naibu Waziri huyo kuangalia mipaka hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad
Masauni (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji
Mkoa wa Kilimajaro alipotembela mpaka wa Tarakea wilayani Rombo Naibu waziri
Masauni amesema kuwa licha ya changamoto zinazojitokeza katika mipaka yote
miwili ni lazima kuendelea kuimarisha ulinzi kwenye mipaka hiyo na kudhibiti
njia zote zisizo rasmi zinazotumiwa na wahamiaji haramu pamoja na
wafanyabiashara za magendo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad
Masaun akionyeshwa Mpaka katika picha unaotenganisha Tanzania na Kenya ulioko
Holili wilayani Rombo alipofanya zaiara ya siku moja ya kikazi kuangalia mipaka
hiyo na kutoa maelekezo kwa wahusika wa kulinda mipaka hiyo namna ya kuweza
kukabilina na changamoto zilizopo katika mpaka huo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad
Masaun akipewa maelezo na Afisa Mipaka Holili Michel Amo, juu ya jiwe linaloonyesha mpaka wa Tanzania na Kenya
lililopo katika mpaka wa Holili ambalo limekua likisogezwa na watu
wasiojulikana hivyo kuharibu alama za mipaka. Naibu waziri Masauni amesema kuwa
licha ya changamoto zinazojitokeza katika mipaka yote miwili ni lazima
kuendelea kuimarisha ulinzi kwenye mipaka hiyo na kudhibiti njia zote zisizo
rasmi zinazotumiwa na wahamiaji haramu pamoja na wafanyabiashara za magendo.
.....................................................................................................
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad
Masauni avitaka vyombo vya ulinzi na usalama nchini kuzidi kuimarisha ulinzi katika
mipaka ili kushirikiana na Serikali katika mpango wa kupambana na uhalifu nchini.
Masauni aliyasema hayo leo wakati alipofanya
ziara katika mipaka ya Tarakea na Holili
iliyopo mkoani Kilimanjaro ili kujione changamoto zinazojitokeza katika mipaka
hiyo ambapo tarifa zinaonyesha kwamba kuna njia zisizo rasmi zaidi ya 265
zinazotumiwa kuptisha bidhaa za magendo na wahamiaji haramu
Katika ziara hiyo Naibu Waziri Masauni
alivitaka vyombo vyote vya ulinzi na Usalama nchini kuhakikisha vinaashirikiana
kila mtu kwa nafasi yake ili kupambana na uhalifu wa kupitisha bidhaa za
magendo zinazopitishwa katika mipaka hiyo na kuikosehsa serikali mapato.
Masauni alisema kuwa Serikali ya awamu ya
Tano ina dhamira ya kupeleka nchi katika uchumi wa kati hivyo ni lazima kwa
vyombo hivyo kudhibiti biashara zote zinazopita kimagendo mipakani humo lakini
pia kuepuka rushwa ili kupiga hatua mbele za kimaendeleo.
Pamoja na kuwapo kwa changamoto ya nguvu kazi
na vitendea kazi serikali itahakikisha inaaandaa maofisa wa kutosha mipakani
humo ili kuongeza nguvu kazi wakati wa operesheni zao na doria wakati wote.
Aidha Masauni ametoa rai kwa watumishi wa
vyombo hivyo kujiepusha na tabia ya kushirikiana au kuwaficha wafanyabiaashara
wanao jihusishaa na biashara ya maagendo.
Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Kilimaanjaro Kamishna Msaidizi Mwqaandanizi Wilbrod Muutafungwa almueleza naibu
Waziri huyo licha ya changamoto zilizopo wanaendelea kuimarisha ulinzi katika
maeneo yote ya mipaka kwa kufanya doria mara kwa mara licha ya kwamba
wafanyabiashara hao wa bidhaa za magendo kutumia mbinu mbalimbali kukwepa
ushuru lakini Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limeweza kuwatia mbaroni.



