Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alipowasili katika Gereza Kuu
la Karanga, Mkoani Kilimanjaro wakati alipotembelea kiwanda cha viatu kilichopo gerezani haapo
ili kujionea uzalishaji wa bidhaa mbalimbali hasa viatu. Naibu Waziri huyo
amelitaka Jeshi hilo kuzidi kuboresha bidhaa za viatu hivyo ili kujipatia soko
kubwa ndanni ya nchi na kutekeleza agizo la Rais Magufuli kuhakikisha majeshi
yote nchini yanattumia viatu vinavyotengenezwa na Jeshi la Magereza.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad
Masauni akisalimiana na Mkuu wa Gereza
la Karanga, Kamishna Msaaidizi Mkwiche
mkoani Kilimanjaro wakati alipofanya ziara katikaa Kiwanda cha viatu
kilichopo katika gereza hilo ili kujionea
uzalishaji wa bidhaa za viatu ambavyo Rais Magufuli alitaka majeshi yote
nchini kutumia viatu vinavyotengenezwa na Jeshi la Magereza.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad
Masauni akisikiliza maelezo kuhusu uzalishaji wa viatu katika kIwanda cha
Gereza la Karanga kutoka kwa Fundi Mkuu wa Kiwanda hicho Ali Jambaraga wakati
alipofanya ziara yake kwenda kujionea uzalishaji wa bidhaa mbalimbali lakini
pia ametaka wazidi kuzalisha bidhaa bora zaidi ili kuteka
soko la ndani na je ya nchi ikiwa ni pamoja na kutekeleza agizo la Rais
Magufuli kuhakikisha majeshi yote nchini kutumia viatu vinavyotengenezwa na
Jeshi la Magereza.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad
Masauni akijionea kiatu aina ya Safari
buti kinachozalishwa na Kiwanda cha Karanga kilichopo Mkoani Kilimanjaro wakati
akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja kiwandani katika Mkoa huo. Masauni
amesisitiza kiwanda hicho kuzalisha bidhaa bora zaidi ili kuteka soko kubwa
zaidi pamoja na kutekeleza agizo la Rais Magufuli kuhakikisha majeshi yote
nchini yanatumia viatu vinavyozalishwa na Jeshi hilo. Kulia ni Mkuu wa Kiwanda
hicho Mrakibu Msaidizi, Michel Minja na kushoto ni Ali Jambaraga Fundi Mkuu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad
Masauni akiangalia kiatu kilichokuwa tayari kuvaliwa kilichotengenezwa katika
kiwanda cha Karanga kilichopo Gereza Kuu
la Karaga mkoani Kilimanjaro. Naibu Waziri huyo amesisitiza Jeshi hilo kuzidi
kutengeneza bidhaa bora zaidi za viatu ili kuhakikisha wanapata soko kubwa
ndani nan je ya nchi., kulia ni Kamishan Msaidizi Mwandamizi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa
aliye aambatana nae kwenye ziara hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad
Masaun (aliyevaa koti) akitoa maelekezo kwa Wakuu wa Gereza la Karanga na
kiwanda cha Viatu kilichopo gerezani hapo. Masauni amelitaka jeshi hilo kuzidi
kutoa bidhaa bora ili kuendelea kuteka soko kubwa ndani nan je ya nchi.
.................................................................................................
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad
Masaun aagiza Jeshi la Magereza kuzidi kuboresha viatu vinavyotengenezwa na
kiwanda chao ili kujipatia soko kubwa ndani ya nchi na nje.
Hayo aliyasema jana kwa wakuu wa Gereza la
karanga na viongozi wa kiwanda hicho alipofanya ziara yake ya siku moja katika
kiwanda cha viatu kilichopo katika gereza hilo, mkoani Kilimanjaro
Aidha, Naibu Waziri huyo alisisistiza Jeshi
hilo kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kuhakikisha majeshi yote nchini
yanatumia viatu vinavyozalishwa na Jeshi la Magereza, hivyo ni muhimu kuendelea
kuzalisha bidhaa zilizo bora zaidi
Haiingii akilini maofisa wa majeshi
mbalimbali nchini kuagiza viatu nje ya nchi wakati viwanda vya ndani vinauwezo
wa kuzalisha viatu bora zaidi vinavyodumu kwa muda mrefu kuliko vinavyoagizwa
kutoka nje ya nchi, alisema Masauni.
Masauni alisema kwamba dhamira ya Serikali ya
awamu ya tano ya kuipeleka nchi katika uchumi wa kati hivyo Jeshi la Magerezaa
kupitia kiwanda chake na miradi mingine mingi halina budi kuendelea kuzidisha
kuzalisha viatu bora vitakavyo kidhi kiwango cha uhitaji na soko ili kukuza
uchumi wao na Serikali kwa ujumla.
Aidha, katika ziara yake, Naibu Waziri
Masauni amesisitiza kuwa ni muhimu Jeshi hilo kufanya miradi mingi kwa ustadi
mkubwa ili kujipatia psa zitakazosaidia kujiendesha wao kama jeshi na mashirika
mengine yanayounga mkono miradi yao hivyo kutotegemea ruzuku kutoka serikalini.
Waziri
huyo alilipongeza Jeshi hilo kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora kulinganisha na
nyingine zinazoingizwa nchi, hivyo amesisitiza kuzidi kutengeneza viatu bora
zaidi ili kuwa na uwanja mpana wa soko la ndani nan je ya nchi.





