Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuutaarifu umma kuwa, kwa mujibu wa vifungu
vya 8 na 16 vya Sheria ya Ushuru wa Bidhaa Sura ya 147, wazalishaji wote wa
bidhaa zinazotozwa Ushuru wa Bidhaa na wazalishaji wa malighafi ya kutengenezea
spiriti wanatakiwa kusajiliwa na kupewa leseni na Kamishna Mkuu wa TRA kabla ya
kuanza uzalishaji. Bidhaa zinazotozwa Ushuru wa Bidhaa zimeainishwa katika
jedwali la nne la Sheria husika. Baadhi ya bidhaa hizo ni kama Bia, Sigara,
Spiriti, Mvinyo na Vinywaji baridi.
Masharti
ya Leseni
1)
Maombi
yote yatumwe kwa Kamishna Mkuu kwa kutumia fomu ya maombi ya leseni
inayopatikana katika ofisi za TRA au tovuti: www.tra.go.tz
2)
Maombi
tofauti yafanywe kama ifuatavyo:
a)
Kwa
kila kiwanda ambacho kitatumika kuzalisha bidhaa. Leseni itatumika kwa kiwanda kilichopewa
leseni pekee
b) Kwa kila aina ya bidhaa itakayozalishwa
na leseni itatumika kuzalisha bidhaa husika pekee.
3)
Mmiliki
wa leseni hataruhusiwa kuhamisha umiliki wa leseni husika, kubadili kiwanda au
kuzalisha bidhaa tofauti katika kiwanda kilichopewa leseni bila kufanya maombi
na kuruhusiwa na Kamishna Mkuu.
4)
Baada
ya kupewa leseni, mzalishaji anatakiwa kumjulisha Kamishna Mkuu juu ya tarehe
ya kuanza uzalishaji ndani ya siku 21 tangu uzalishaji huo kuanza.
5)
Pindi
bidhaa yoyote inapoamuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Bunge kuanza kutozwa Ushuru
wa Bidhaa, mzalishaji wake anapaswa kumjulisha Kamishna Mkuu na kuomba leseni
ya uzalishaji ndani ya siku 21 baada ya bidhaa husika kuanza kutozwa Ushuru wa
Bidhaa.
6)
Leseni
ya uzalishaji itakwisha muda wake kila tarehe 31 Disemba ya mwaka ambapo
mmiliki atatakiwa kuomba leseni mpya.
7)
Wazalishaji
wa spiriti yenye vionjo na isiyo na vionjo (Denatured and Undenatured Spirit)
pia wanatakiwa kuomba leseni za uzalishaji kwa Kamishna Mkuu.
Uzalishaji
wa bidhaa zinazotozwa Ushuru wa Bidhaa bila ya leseni ni kosa linalopelekea
adhabu ya faini au kifungo au faini na kifungo ikiwa ni pamoja na kutaifishwa
kwa mitambo na bidhaa zote zilizohusika katika utendaji wa kosa hili.
Wazalishaji wote wanaaswa kumiliki leseni halali katika wakati wote wa
uzalishaji na TRA kwa kushirikiana na wadau wengine wataendesha ukaguzi
endelevu kuhakiki matakwa haya ya sheria.
Waombaji
wanatakiwa kufanya maombi katika ofisi yoyote ya TRA ambako viwanda husika
vinapatikana ili kuepuka adhabu kali zinazotokana na ukiukwaji wa matakwa haya
ya sheria.
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”
Limetolewa
na:
Idara
ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA-Makao
Makuu
Dar
es Salaam