
Mjumbe wa heshima wa Shirikisho la Soka Afrika,Said El Maamry
...........................................................
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Mjumbe wa heshima wa Shirikisho la Soka Afrika,Said El Maamry anatarajia kuwakutanisha viongozi wa Simba na Yanga ili kumaliza utata wa beki Hassan Ramadhani Kessy na kuotoa mgogoro uliopo katika usajili kwa pande zote mbili.
El
Maamry anakutana na pande hizo mbili kujadili suala la beki Hassan
Kessy ambaye Simba inamlalamikia kusajili na Yanga huku akijua ana
mkataba na wana msimbazi na Kessy anailalamikiwa Simba.
“Kweli
El Maamry amekubali na leo, ndiyo tunakutana kwa ajili ya kulimaliza
suala hilo na Simba,” alisema mmoja wa viongozi wa Yanga kutoka makao
makuu ya Yanga, Jangwani jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa Lengo letu ni kulimaliza hili suala, kwa kuwa hii nafasi
ya El Maamry ni nzuri kwa maana hiyo ya kulimaliza, tunaamini tutafikia
mwafaka na kumuacha mchezaji akili yake awaze mpira tu na sio mambo
mengine.
Kamati
ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ambayo inashughulikia suala
hilo, ilitoa nafasi kwa Yanga na Simba kufikia mwafaka kabla yenyewe
haijatoa maamuzi.
Lakini
kama Yanga itashindwa na kuamliwa kulipa, itakuwa tatizo kwao kwa kuwa
tayari imeshamtumia Kessy katika mechi kadhaa za ligi kwa upande
mwingine msemaji wa TFF alishawahi kusema kuwa ishu ya Kessy sio usajili
na kuwaondoa mashabiki wa Yanga kuwa hawawezi kukatwa pointi zozote
kwani usajili wake ulipitishwa.
Beki huyu ameingia matatani na klabu yake ya zamani yaani Simba kwa madai kuwa alivunja mkataba na kujiunga na Yanga huku akijua kabisa ni kosa hivyo kamati itatoa uamuzi sahihi na sio wa kukomoana hekima na busara zitatumika kumaliza suala hilo ambalo limekuwa ngumzo kwa wadau.
Beki huyu ameingia matatani na klabu yake ya zamani yaani Simba kwa madai kuwa alivunja mkataba na kujiunga na Yanga huku akijua kabisa ni kosa hivyo kamati itatoa uamuzi sahihi na sio wa kukomoana hekima na busara zitatumika kumaliza suala hilo ambalo limekuwa ngumzo kwa wadau.
Baada
ya kamati hiyo kukaa na kupata maamuzi, iliona inawezekana pia Yanga na
Simba kukutana na kulimaliza suala hilo badala ya kutoa maamuzi ambayo
yatakuwa yanauumiza upande mmoja
0 Comments