Mtendaji Mkuu
TEMESA Dr. Mussa Mgwatu (wa pili kushoto) akisikiliza Kaimu Meneja wa TEMESA
Kagera Bw. Wilson Nyitwa(wa pili kulia) alipotembelea ofisi hiyo na kuzungumza na
baadhi ya watumishi wa TEMESA Kagera kushoto ni Msaidizi wa Meneja wa TEMESA
Kagera Bw. Charles Mbegete na kulia ni Mhasibu
Bi. Joviness Samson.
Mtendaji
Mkuu TEMESA Dr. Mussa Mgwatu (katikati) akikagua chumba maalumu kwa ajili ya
injini (Engine Room) kulia ni msaidizi wa Meneja Bw. Charles Mbegete na kushoto ni Kaimu
Meneja TEMESA Kagera Bw. Wilson Nyitwa.
Mtendaji
Mkuu TEMESA Dr. Mussa Mgwatu (wa tatu kushoto) akiongea na baadhi ya watumishi
wa TEMESA Kagera alipotembelea kituoni hapo kukagua jinsi Ofisi inavyofanya
kazi na kuzungumza na wafanyakazi.
Picha Na Theresia
Mwami TEMESA (Kagera).
............................................................................................
Na
Theresia Mwami TEMESA Kagera
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu amewataka watumishi
wake kuacha kufanya kazi kwa uzembe na mazoea badala yake waongeze ubunifu
katika miundombinu iliyopo ili kuweza kuzalisha zaidi ikiwa ni sanjali na
kuweka mikakati madhubuti ya kukusanya madeni siku hadi siku.
Ameota
agizo hilo alipotembelea na kujionea hali ya karakana ya TEMESA mkoani Kagera
na kumuagiza Kaimu Meneja wa TEMESA Kagera Bw.Wilson Nyitwa kusimamia kwa
makini utekelezaji wa majukumu ya Wakala huo mkoani hapo.
“Inatupasa
kuanza na hiki kidogo tulicho nacho kwa kuziba mianya ya uzembe na muongeze
uadilifu na ufuatiliaji katika kazi tulizo nazo tufanikishe utendaji wa kazi
zetu” alisema Dkt. Mgwatu.
Dkt
Mussa Mgwatu ameongeza kuwa watendaji wanapaswa kupambana ili kulinda soko
lililopo kwa sasa na hata kuongeza wateja zaidi. Kwa sasa wateja wa TEMESA ni
taasisi za serikali ambazo zinapeleka magari na mitambo kutengenezwa katika
karakana zao.
Aidha
kwa upande wake Kaimu Meneja wa TEMESA
Kagera Bw.Wilson Nyitwa alieleza kuwa Kituo chake mbali na kuwa na karakana na kutengeneza
magari na vifaa vya umeme,kukodishaji mitambo na usimikaji umeme katika majengo
mbali mbali ya serikali pia kinasimamia uendeshaji wa vivuko viwili vilivyopo
Kyanyabasa na Ruvuvu.
Alieleza
kuwa TEMESA Kagera ina changamoto nyingi zikiwemo uchakavu wa Karakana yake
iliyojengwa tangu mwaka 1958 pamoja na kukosa vitendea kazi muhimu pamoja na
magari kwa ajili ya matumizi ya ofisi lakini bado wanafanya kazi kwa kujituma na
kuzalisha zaidi ya Shillingi Million 50 kwa mwezi.
“Nakuomba Mtendaji Mkuu utusaidie gari moja
kwa ajili ya matumizi ya kituo nyongeza ya mafundi, vitendea kazi vya kisasa
vya karakana ,ukarabati wa karakana ya mkoa ili kutuwezesha kutekeleza majukumu
yetu na kuzalisha zaidi.
Mtendaji
Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yupo katika ziara ya kikazi Kanda ya Ziwa na
atatembelea vituo vya TEMESA vilivyopo ili kubaini changamoto na kujionea
utendaji kazi wa vituo hivyo na kwa kuanzia yupo Mkoani Kagera.


