Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umepokea
ugeni kutoka Wizara ya Afya ya Zanzibar katika ziara ya mafunzo
iliyoongozwa na Mh.Mahamud Thabit Kombo ambaye ni Waziri wa Afya wa
Zanzibar.
Katika ziara hiyo, yenye lengo la
kushiriki uzoefu wa utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo, Waziri na timu
yake walipata melezo na kujionea shughuli mbalimbali za Mfuko huo.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, Mh.Kombo alisema "tunahitaji kujifunza kutokana
na uzoefu wenu wa kuendasha Mfuko wa bima ya afya, hatukuona haja ya
kwenda mbali kwani tuna kaka na dada zetu hapa karibu na wana uzoefu wa
kutosha".
Mh. Kombo alisema kuwa Wizara ya Afya
ya Zanzibar ina ushirikiano mkubwa sana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto na kusisitiza kuwa Wizara hizi zinafanya
kazi kwa karibu sana na hii inasaidia kufanikisha maendeleo ya sekta ya
afya kwa pande zote.
Akiwakilisha
mada ya Utekelezaji wa shughuli za Mfuko,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF
Bw. Bernard Konga aliongelea umuhimu wa Bima ya Afya katika maendelea ya
sekta ya afya nchini na kuanisha utekelezaji wa majukumu ya Mfuko huo
ambapo alielezea pia mifumo imara ya uendeshaji wa Mfuko ikiwemo ya
Tehama lakini pia mifumo ya kubaini udanganyifu ili kuudhibiti.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne Makinda (Spika Mstaafu) lielezea
umuhimu wa Mfuko kujipanga kimuuondo katika kuhakikisha unaweza kufikia
azma ya Serikali ya kuhakikisha afya bora kwa wote. "Pamoja na mambo
mengine, elimu kwa umma ni suala la msingi sana katika utekelezaji wa
shughuli za Mfuko na kuwapa nafasi wadau kuuliza na kujibiwa hoja
zao"alisema.
Akitoa shukrani zake kwa NHIF
katika ziara hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Mganga Mkuu wa Serikali
Prof. Muhammed Bakari, Waziri Kombo alishukuru Mfuko na kusema kwamba
utabakia kwenye historia ya maendeleo ya sekta ya afya Zanzibar lakini
pia alisisitiza umuhimu wa kuwa na bima ya afya kwa kusema "Bima ya afya
ni Mkombozi wa wanyonge"
Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit Kombo akizungumza na
viongozi mbalimbali wa NHIF kuhusu kujifunza kutokana na uzoefu wa
kuendasha Mfuko wa bima ya afya, katika ziara ya mafunzo makao makuu ya
NHIF leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bi.
Anne Makinda (Spika Mstaafu).
Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne Makinda (Spika Mstaafu) akitoa
maelezo mafupi kuhusu shughuli za Mfuko leo makao makuu ya mkuko jijini
Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit
Kombo
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga akitoa maelezo mafupi
kuhusu shughuli za Mfuko leo makao makuu ya mkuko jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit Kombo.
Meneja Wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Elentruda
Mbodoro akitoa walezo mafupi kwa Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud
Thabit Kombo kuhusu utunzaji wa nyaraka za wanacha wa mfuko huo leo
jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit Kombo akiagana na Mwenyekiti
wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne Makinda (Spika Mstaafu) leo alipo tembelea
Makao makuu ya mfuko huo.
Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit Kombo
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa NHIF leo makao
makuu jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
.......................................................................................................................






