MLIZI wa kutumainiwa kwenye kikosi cha Mbeya City fc, Hassan
Mwasapili amewataka mashabiki wa timu yake kutulia na kutokuwa na hofu
yoyote na mchezo ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Simba Sc
uliopangwa kuchezwa jumatano hii kwenye uwanja wa Sokoine jijini
hapa.
Akizungumza na mbeyacityfc.com mapema leo, Mwasapili aliweka wazi
kuwa hana presha yoyote na mchezo wa jumatano kwa sababu anaifahamu
vizuri Simba hasa ukizingatia kuwa huu utakuwa ni mchezo wake wa tano
kucheza dhidi ya timu hiyo tangu kupanda daraja kwa kikosi cha Mbeya
City.
“Huu utakuwa mchezo wangu wa tano kucheza dhidi ya Simba
Sc,naifahamu vizuri najua nguvu yao iko kwenye eneo gani la uwanja,
siwezi kusema mengi juu ya matokeo yao msimu huu ni hakika wameanza
vizuri lakini kuna jambo moja muhimu kuwa mechi zote waalizoshinda
wamecheza nyumbani, jumatano hii huu ni wakati wao mgumu zaidi kwa
sababau sasa wanacheza ugenini na hii ndiyo nafasi yetu sisi kupambana
nao na kuwafunga” alisema.
Akiendelea zaidi Mwasapili alitanabaisha kuwa,matokeo ya pointi nne
kwenye michezo miwili ya City iliyopita yametosha kuhifadhi nguvu za
kutosha kukabiliana na kikosi cha Simba Sc hivyo hakuna shaka yeyote
kuwa nafasi ya ushindi ipo kwa timu yake amabayo itakuwa ikicheza kwa
nguvu zote kutokana na uwepo wa sapoti ya mashabiki.
“Tumekuwa na matokeo mazuri michezo miwili iliyopita, hakunaa shaka bado tuna morali ya kutosha, tuko tayari kukabiliana nao na tutawasimamisha,kitu muhimu naomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya sapoti, nasi tutacheza kwa uwezo wetu wote imani yangu kuwa hatutawaangusha hivyo watulie na wasiwe na hofu yoyote”, alimaliza.