Mkurugenzi wa Global Publishers Bw.Erick
Shigongo (mgeni rasmi) akisalimiana na wachezaji kabla ya mchuano mkali
nawakuvutia wakati wa Tamasha la Michezo la kuadhimisha Siku ya Nyerere Nchini
lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es salaam tarehe 14.10.2016. Ushindi
ulienda kwa wenye sare Nyekundu kwa mikwaju ya Penati baada ya kutoshana nguvu
ya 2-2 katika muda wa kawaida.
Picha ya pamoja ya Timu iliyoibuka washindi
wakati wa Tamasha la Michezo la kuadhimisha Siku ya Nyerere Nchini
lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dare es salaam tarehe 14.10.2016. Ushindi
ulipatikana kwa mikwaju ya Penati baada ya kutoshana nguvu ya 2-2 katika muda wa kawaida.
Baadhi ya wachezaji wa timu iliyoibuka mshindi
wakishangilia baada ya kupachika bao la kusawazisha katika dakika mbili za
mwisho na kufanya mchezo kuwa 2-2 na kisha kuingia katika mikwaju ya penati
zilizowa ushindi wachezaji wenye uzi mwekundu wakati wa Tamasha la Michezo
katika kuadhimisha siku ya Nyerere nchini lililofanyika ndani ya gereza la
Ukonga jijini Dar es salaam tarehe 14.10.2016
Kepteni wa Timu iliyoshinda Johnson Nguza (Papii
Kocha) akibeba kombe kwa niaba ya timu yake baada ya kulipokea toka kwa Mgeni
Rasmi Erick Shigongo wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha siku ya
Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dar es salaam, tarehe 14.10.2016
Johnson Nguza aka Papii Kocha akitumbuiza kwa
pamoja na wanamuziki wa Twanga Pepeta wakati wa Tamasha la Michezo katika
kuadhimisha siku ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani Ukonga jijini Dar es
salaam, tarehe 14.10.2016
Sehemu ya zawadi zilizoletwa na wageni gerezani
wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha siku ya Nyerere Nchini lililofanyika
gerezani humo tarehe 14.10.2016
Baadhi ya viongozi wa Jeshi la Magereza na
wageni mbalimbali wakishiriki chakula cha mchana pamoja na wafungwa (hawapo
pichani) gerezani Ukonga wakati wa Tamasha la Michezo katika kuadhimisha siku
ya Nyerere Nchini lililofanyika gerezani humo
tarehe 14.10.2016.
Picha zote na Deodatus
Kazinja wa Jeshi la Magereza
...................................................................................................................
Na ASP Deodatus Kazinja
wa Jeshi la Magereza
Katika kuadhimisha miaka
17 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere Gereza Kuu Ukonga kwa
kushirikiana na Kampuni ya Global Publishers limefanya Tamasha la michezo
mbalimbali kwa wafungwa wa gereza hilo.
Akiongea katika Tamasha
hilo Mkurugenzi wa Global Publishers aliyekuwa pia mgeni rasmi Bwana Erick
Shigongo amewaambia wafungwa kuwa dhimra ya ujio wao gereza ni katika kuonesha
kuwathamini, kuwahurumia na kuwatia moyo kwamba kuwa kwao gerezani siyo kwamba
wametengwa na dunia.
Bwana Shigongo aliwatia
moyo wafungwa hao kuwa hawatakiwi kukata tamaa na bado wanayo nafasi ya
kubadilika na kuwa raia wema. “Kila mwanadamu anaowajibu wa kubadili maisha yake,
Mwalimu Nyerere tunayemuadhimisha leo alizaliwa kama mimi na wewe na
kutengeneza maisha yake na leo tunamkubuka kwanini wewe ushindwe?”
Aliongeza “ najua wengi
wenu mko hapa mkiwa mmeitwa majina mengi kwakuwa mmehukumiwa, hizini hukumu za
wanadamu, mnaouwezo wa kuandika kurasa mpya katika maisha yenu na siku mkitoka
duniani waseme mtu mwema ameondoka. Siku moja inatosha kubadili maisha yako,
kila siku andika ukurasa mpya wa maisha yako na Mungu atakuongoza alisisitiza
Shigongo.
Wadau wengine
walioungana na Global Publishers katika tukio hilo ni pamoja na Tume ya Haki za
Binadamu Nchini ikiongozwa na mwenyekiti wake Thom Nyanduga na ndugu Rajab
Maranda (aliyewahi kuwa mfungwa gereza Ukonga) ambao kwa pamoja walileta zawadi
mbalimbali kwa wafungwa hao ikiwemo vifaa vya, sabuni,soda kikombe ambacho
kilitolewa kwa timu iliyofanya vizuri katika mpira wa miguu.
Katika Tamasha hilo
wafungwa walishiriki michezo ya kukimbia katika magunia, kukimbia na yai katika
kijiti, mbio za mita 100 vijana kwa wazee, mita 400 kupokezana vijiti, kuvuta
kamba, mieleka, mpira wa miguu, mashairi, kuonesha vipaji vya uchekeshaji,
kuimba kwa mtindo kufokafoka, ngoma za jadi
na burudani kwa kushirikiana na baadhi ya wanamuziki wa bendi ya Twanga
pepeta.







0 Comments