Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Gerson
John Mdemu akikakagua timu za mpira wa miguu za wafanyakazi wa Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakati wa Bonanza kwa ajili ya kumuenzi Baba wa
Taifa leo Jijini Dar es Salaam, Mechi zilikuwa ni baina ya timu ya wafanyakazi
Mawakili na wasio mwawakili ambapo mechi ilimalizika kwa mawakili kulala kwa
mikwaju ya penalti 4 kwa 2.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Gerson
John Mdemu akizungumza na wachezaji wa mpira wa Pete kutoka timu za wafanyakazi
wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakati wa Bonanza kwa ajili ya
kumuenzi Baba wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha timu ya mpira wa miguu ya wafanyakazi wa Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa kada za kawaida kabla ya kuanza Bonanza kwa
ajili ya kumuenzi Baba wa Taifa leo Jijin Dar es Salaam.
Kikosi cha
timu ya mpira wa miguu ya wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali wa kada ya Uwakili wakiwa katika pozi kabla ya kuanza Bonanza kwa
ajili ya kumuenzi Baba wa Taifa leo Jijin Dar es Salaam.
Menejimenti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali wakishindana kukimbia kwa maguni wakati wa Bonanza kwa ajili ya
kumuenzi Baba wa Taifa lililofanyika katika viwanja vya Shule Kuu ya Sheria,
leo Jijin Dar es Salaam.
Mshindi wa kukimbia kwa gunia katika timu ya
Menejimenti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Asiatu Msuya
akishangilia kwa furaha mara baada ya kumaliza mbio hizo akiwa mshindi wakati
wa Bonanza kwa ajili ya kumuenzi Baba wa Taifa leo Jijin Dar es Salaam.
Timu za wanawake na wanaume za kuvuta kamba za
wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakivutana wakati wa
Bonanza kwa ajili ya kumuenzi Baba wa Taifa lililofanyika katika viwanja vya
Shule Kuu ya Sheria, leo Jijin Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali wakicheza Karata na Draft wakati wa Bonanza kwa ajili ya
kumuenzi Baba wa Taifa lililofanyika katika viwanja vya Shule Kuu ya Sheria,
leo Jijin Dar es Salaam.
Wachezaji wa Netboli wakionyeshana ubavu wakati
wa mechi baina ya wafanyakazi wakike Mawakili na Wasio mawakili. Hadi mechi
inaisha mawakili walikuwa mbele kwa idadi ya magori 5 -1.
Wachezaji
wa mpira wa miguu wanaume wakionyeshana ubavu wakati wa mechi baina ya
wafanyakazi mawakili na wasio mawakili wakati wa Bonanza kwa ajili ya kumuenzi
Baba wa Taifa leo Jijini Dar es Salaamhadi mechi inamalizika wafanyakazi wa
kada za kawaida waliibuka kidedea kwa jumla ya mikwaju ya penati 4 kwa 2.
Picha
na: Frank Shija, MAELEZO












0 Comments