Rais
wa Chama cha wafamasia Tanzania (PST) Ndg. Michael Kishiwa (aliyesimama)akitoa
taarifa ya Chama kwa kifupi kwa Mgeni
Rasmi Mhe. Mrisho Gambo katika Kongamano la 49 la wafamasia Tanzania
linalofanyika Jijini Arusha.
Wanachama
wa PST wakifuatilia ufunguzi wa Kongamano
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo akitoa hotuba katika ufunguzi wa
kongamano la 49 la Chama cha Wafamasia
Tanzania
Wajumbe
wa kongamano wakiendelea kufuatilia Hotuba ya Ufunguzi
1Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo(Kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Chakula na dawa Hiti Silo katika Kongamano la wafamasia
linalofanyika katika Jiji la Arusha.
....................................................................................................
Na Nteghenjwa Hosseah, ARUSHA
SERIKALI imesema kuwa inaanza kufanya maboresho
kwa kuandaa na kuhakikisha Sera ya Uboreshaji wa Viwanda vya Dawa
vilivyopo nchini kwa kuwawezesha na kuwajengea uwezo wenye viwanda
nchini ili waweze kuzalisha dawa na kupunguza uagizaji wa dawa kutoka nje ya
nchi.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo kwa niaba ya Waziri wa Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama alipokuwa akizungumza katika
Kongamano la 49 la Chama Cha Wafamasia Tanzania (PST),linalofanyika
jijini hapa kwa siku mbili.
Akizungumza kwa niaba ya Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mrisho Gambo,alisema kuwa kutokana na umuhimu wa sekta hiyo ya dawa, Serikali
inaangalia taaluma hiyo kwa macho mawili kwa lengo la kuiboresha ili iweze
kutoa huduma bora.
"Wizara yangu inaangalia taaluma hii kwa
macho mawili katika kuhakikisha kuwa sekta ya dawa inaboreka na inakua na
hatimaye kuweza kukuza uchumi wetu, kwa kuwawezesha na kuwajengea uwezo wenye
viwanda nchini ili waweze kuzalisha zaidi ikiwa ni pamoja na kuwahakikishia
soko ndani ya nchi na kupunguza uagizaji wa dawa kutoka nje ya nchi na hivyo
kuwa na dawa bora, salama na zenye ufanisi"
"Endapo tutazalisha dawa zetu wenyewe hii
itatupunguzia gharama zisizo za lazima kuagiza dawa nje ya nchi, sambamba na
hili pia tunaboresha vyuo vya Wafamasia ili waweze kutoka wataalamu bora wa
masuala haya ya madawa,”alisema Gambo
Akizungumzia suala la wizi wa dawa katika hospitali
za serikali,alisema kuwa Serikali haina mchezo na yoyote atakayokiuka maadili
ya taaluma hiyo na kuwa watawachukulia hatua kali za kisheria ili wananchi
wapate huduma bora za dawa.
"Mbali na changamoto ya upungufu wa dawa, wafanyakazi
wasio waadilifu ambao wanatumia nafasi zao vibaya wanashirikiana na baadhi ya
wafanyabiashara na kuuza dawa, hili ni suala muhimu PST jadilianeni suala
la maadili kwani hatua za kisheria dhidi yao zitachukuliwa"alisema
Awali Rais wa PST, Michael Kishiwa, aliiomba Serikali
kuongeza udahili wa wanafunzi wa famasia wakiwemo mafamasia wasaidizi ili
kutoa dawa sahihi kwa wagonjwa.
Alisema hivi sasa idadi ya watanzania ni kubwa,
lakini wataalamu wa dawa Wafamasia ni 1,200, hali inayochangia kuwepo kwa watoa
huduma hiyo wasio na sifa.
Alisema kutokana na kukosekana wanataaluma
kumekuwepo na changamoto kubwa ya baadhi yao kukiuka maadili na wengine kufanya
kazi ya utoaji dawa pasipokuwa na uelewa nayo, hali ambayo hatari kwa afya za
binadamu.
Kishiwa alisema kazi kubwa ya chama chao
kuhakikisha inasimamia ubora wa utoaji huduma ya dawa na kusimamia maadili, ili
wananchi wapate dawa sahihi na kuzitumia ipasavyo.
“Tunashirikiana na baraza la usajili la wafamasia
katika kukemea vitendo hivyo vya ukiukwaji wa maadili na ndiyo maana tunaiomba
serikali iongeze udahili na vyuo vinavyotoa taaluma hii"alisema
Naye Msajili wa Baraza la Wafamasia, Elizabeth
Shekalage alisema kwa sasa wananchi wengi wamechukulia huduma ya dawa ni
biashara na kuwa baraza limejipanga kupambana na watu wanaofanya huduma hiyo ni
biashara huku wakikiuka maadili.
"Uchache wa wanataaluma unasababisha kika
mtu aone hii ni biashara huria na yeyote anaweza kuifanya,kuna uhaba mkubwa wa
fundi dawa sanifu,mafundi dawa wasaidizi,dawa ni sumu hivyo tunasimamia hili
ili kuepusha madhara kwa watumiaji"alisema Elizabeth
Kongamano la Mwaka huu linaenda na kauli mbiu
isemayo kuelezea ubora,usalama,ufanisi na upatikanaji wa huduma bora za
kifamasia.





0 Comments