Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Gabriel Daqarro akizungumza
na Maafisa watendaji wa Kata wa Jiji la Arusha (Hawapo Pichani) wakati wa kikao
maalumu na watendaji hao kilichofanyika miwshoni mwa juma jijini hapa.
Mwenyekiti wa Maafisa watendaji wa Kata na Mtendaji wa Kata ya
Kati Ndg. Suleimani Kikingo akichangia wakati wa Kikao na Mkuu wa Wilaya ya
Arusha
Maafisa Watendaji wa Kata waliohudhuria Kikao na Mkuu wa Wilaya ya
Arusha
Afisa Mtendaji wa Kata ya Levolosi Easter Maganza akitoa ufafanuzi
wa hoja mbalimbali wakati wa kikao
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Gabriel Daqarro(kushoto)
akiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha Ndg. David Mwakiposya wakati wa
kikao na watendaji wa Kata.
.................................................................................................................
Na
Nteghenjwa Hosseah, ARUSHA
Mkuu wa Wilaya ya
Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Gabriel Daqarro mwishoni mwa wiki hii amekutana na
Maafisa Watendaji wa Kata zote za Jiji la Arusha kuzungumzia kuhusu masuala
mbalimbali muhimu yanayotakiwa kupewa kipaumbele katika Wialaya hiii.
Katika Kikao hicho
Dc Daqarro ametilia mkazo masuala ya Usalama wa Chakula katika Mitaa yote,
Ulinzi na usalama, usimamizi wa miradi ya maendeleo pamoja na utoaji wa taarifa
za matukio yasiyo ya kawaida yanayotokea katika kila Kata.
Akizungumza katika
kikao hicho alisema “nahitaji kupata takwimu sahihi kutoka katika kila Kata ya
mahitaji ya Chakula, kiasi kilichopo na namna ambavyo mmejipanga kukabiliana na
upungufu endapo utatokea, kila afisa ugani wa eneo husika ahakikishe anatoa
elimu ya kutosha na kufuatilia kuhusu usalama wa chakula katika eneo lake na
kuwasilisha taariha hizo katika Ofisi yangu.
Sitamuelewa mtendaji ambaye kwa
kutokuwajibika kwake kutasababisha njaa ama upungufu wa chakula kwa namna
yeyote ile.
Aidha alisisitiza kusimamia
miradi ipasavyo ili iwe na ubora na iweze kudumu muda mrefu, kusimamia Usalama
wa Kata kwa kutoa taarifa za kila tukio lisilo la kawaida linalotokea kila siku
na kudhibiti uingiaji wa wageni kutoka nje ya nchi wanaofika katika Kata.
“Wageni wote wa
Nje ya Nchi lazima taarifa zao zifikishwe kwa Afisa uhamiaji wa Wilaya ili
kujiridhisha kwamba wameingia nchini kihalali na kuwa na shughuli maalumu
iliyowaleta katika maeneo yenu aliongeza”.
Sambamba na hilo alisema
si ruhusa kwa Mtendaji wa Kata kutoa mihutasarti kwa ajili ya kumilisha upatikanji wa silaha kwa sababu hivi sasa zoezi hilo
limesitishwa mpaka pale Uhakiki wa silaha utakapokamilka hivyo kwa kuwa
muombaji ni lazima aanzie kwenye ngazi ya kata si ruksa kwa vikao husika kutoa mihutasari ya aina
hiyo.
Mwenyekiti wa
Watendaji wa Kata katika Jiji la Arusha
Ndg. Suleimani Kikingo alisema kwa umoja watahakikisha kwamba maagizo yote
yaliyotolewa wanayatekeleza kwa ufanisi ili kuleta mabadiliko ya haraka na
kutoa hudma bora kwa wakazi wa Jiji hili.





0 Comments