Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella
Manyanya(kulia) akimpa fedha kama zawadi mmoja wa wanafunzi wa Shule ya
Msingi Nyamilima iliyopo Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera kwa kuweza kusoma
na kuandika vizuri wakati alipowatembelea kuwapa pole kwa kukumbwa na
tetemeko la ardhi 4/10/2016.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella
Manyanya (kulia) akimpa mkono wa pole Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi
Ileega iliyopo Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera baada ya Shule yake
kukumbwa na tetemeko la ardhi na kuathiri baadhi ya vyumba vya madarasa
pamoja na nyumba ya Walimu hivi karibuni.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya akihiji katika eneo maarufu la hija
lijulikanalo kama Nyakijoga lililopo Wilayani Missenyi Mkoani Kagera.
PICHS ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM.
......................................................................................................................
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
Serikali imepanga kuijenga shule ya
msingi ileega na kufanya ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa katika shule
ya msingi Nyamilima zote zilizopo wilayani kyerwa mkoani Kagera kufuatia
uharibifu uliotokana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani huko mapema mwezi
September.
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
Serikali imepanga kuijenga shule ya msingi ileega na kufanya ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Nyamilima zote zilizopo wilayani kyerwa mkoani Kagera kufuatia uharibifu uliotokana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani huko mapema mwezi September.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya alipofanya ziara wilayani huko kuangalia athari za tetemeko katika sekta na elimu.
Mhe. Manyanya alisema kuwa kama serikali imejikita katika kurudisha miundombinu ya umma ikiwemo shule ili kuwawezesha wanafunzi kuendelea na masomo kama kawaida.
“Tumeona hali ni mbaya kwenye shule hizi mbili na sisi kama serikali hatuwezi kuliacha suala hili lazima tuzikarabati na kuzijenga zile zinazohitaji kujengwa upya na dhumuni ni kuhakikisha wanafunzi wanaendelea na masomo na kuondokana na changamoto hii: Alisema Mhandisi Manyanya.
Aidha Mhandisi Manyanya amemtaka mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Nyamilima kuacha tabia ya kutoa ruhusa hovyo kwa walimu suala ambalo linaathiri taaluma kwa wanafunzi.
Wakati huohuo Mhandisi Manyanya amesema walimu watakaoshindwa kuwawezesha wanafunzi wao kujua kusoma na kuandika watashushwa vyeo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya alipofanya ziara
wilayani huko kuangalia athari za tetemeko katika sekta na elimu.
Mhe. Manyanya alisema kuwa kama
serikali imejikita katika kurudisha miundombinu ya umma ikiwemo shule ili
kuwawezesha wanafunzi kuendelea na masomo kama kawaida.
“Tumeona hali ni mbaya kwenye shule
hizi mbili na sisi kama serikali hatuwezi kuliacha suala hili lazima
tuzikarabati na kuzijenga zile zinazohitaji kujengwa upya na dhumuni ni
kuhakikisha wanafunzi wanaendelea na masomo na kuondokana na changamoto hii:
Alisema Mhandisi Manyanya.
Aidha Mhandisi Manyanya amemtaka
mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Nyamilima kuacha tabia ya kutoa ruhusa hovyo
kwa walimu suala ambalo linaathiri taaluma kwa wanafunzi.
Wakati huohuo Mhandisi Manyanya
amesema walimu watakaoshindwa kuwawezesha wanafunzi wao kujua kusoma na kuandika
watashushwa vyeo.





0 Comments