![]() |
Jengo hilo lina ofisi za kufanyia
kazi, vyumba vya mikutano vya kutumiwa na Baraza la Amani na Usalama, chumba
cha kuratibia shughuli, maktaba na vyumba vya shughuli za pembeni.
Mwalimu Nyerere, ambaye alikuwa rais
wa Tanzania hadi 1985, alikuwa mmoja wa viongozi waanzilishi wa Muungano wa
Nchi za Afrika (OAU) ambao sasa ni Umoja wa Afrika (AU).
|
![]() |
|
Bi Merkel amezuru nchi kadha za
Afrika zikiwemo Mali na Niger. Hapa anaonekana na Rais Mahamadou Issoufou wa
Niger.
Alishiriki sana katika jitihada za
kuendeleza bara la Afrika na kusaidia mataifa ambayo hayakuwa yamepata uhuru
kujipatia uhuru wake.
Mwalimu Nyerere alipigania sana
kumalizwa kwa ubabe wa Wazungu katika nchi za Rhodesia (sasa Zimbabwe), Afrika
Kusini, na taifa la Kusini Magharibi mwa Afrika/Namibia (sasa Namibia).
|








