
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Baada
ya kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa
CCM Kirumba Mwanza timu ya Toto African 'Wana-kisha mapanda' wametuma
salama kwa wana rambaramba Azam Fc mchezo wao utakaopigwa Jumatano hiii.
Akizungumza
Ramadhani Aiko,ametamba kuwa wana imani kuwa watashinda mechi hiyo
kutokana ushindi wa Mtibwa kuwapa morali wachezaji pamoja na benchi
nzima la ufundi huku wakichangizwa na uwepo wa mashabiki.
"Tunajipanga
kuchukua alama tatu muhimu katika mchezo wetu na Azam hivyo tuna tuma
salama mapema kuwa wajiandaa kula kichapo kwani tulianza kufunga na
Mtibwa goli mbili hata hivyo vijana walijipanga na kupigana na kurudisha
na kupata ushindi wa 3-2"alisema Aiko
Toto
walitoka nyuma ya kufungwa magoli mawili na wakata miwa na waliporudi
walikuja kupigana na hatimaye kushinda hivyo mchezo utakuwa mkali na wa
upinzani kwa timu zote mbili ukiangalia hata Azam nao wametoka kushinda
magoli 3-2 dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba.
Kwa
upande wa Msemaji wa Azam Jafar Maganga,ametamba kuwa nia yao ni kupata
alama tatu na malengo yao ni kuchukua pointi zote tisa wakiwa kanda ya
ziwa na mchezo na Toto watashinda japokuwa sio rahisi.
"Tumejipa
kuwafunga Toto wakiwa hapo kwao kama tuliweza kupata ushindi dhidi ya
Kagera hivyo tunajua wapinzani wetu wanacheza vipi na wakiwa nyumbani
wanaonekana wangumu mpira ni dakika 90 sisi tumejiandaa kushinda
tunasubiri siku ifike tu"alisema Maganga
Azam Fc wanakutana na Toto wakiwa nafasi ya nne wakiwa na alama 19 wakati Toto wao wapo nafasi ya 15 na alama zao 11.
0 Comments